Home Kimataifa Chicago yaendelea kuwa bora, Wachezaji wapya waendelea kuwa mchango

Chicago yaendelea kuwa bora, Wachezaji wapya waendelea kuwa mchango

704
0
SHARE

i

Ikiwa na wachezaji wapya tisa,huku watatu wakiwa ni wa kikosi cha kwanza, Chicago Bulls walitegemewa kuanza taratibu msimu moya wa NBA, lakini hali imekuwa tofauti kidogo na wameanza kwa namna ambayo inaonekana kuleta faraja kwa mashabiki wa klabu hiyo.

Hata hivyo pamoja na kutokuwa mfungaji mzuri au mfungaji wa mara nyingi, mchezaji Rajon Rondo ameendelea kumwagiwa sifa na wachezaji wenzie kwa timu hiyo kuanza vyema msimu huu.

Doug McDermott alifunga pointi 23 points, Jimmy Butler ambaye kwa sasa ndiye anategemewa kuwa kiongozi ndani ya timu hiyo, yeye alifunga pointi 16 huku Rondo akitoa assits 13 na kuiongoza Chicagokupata ushindi wa vikapu118-101 dhidi ya Indiana Pacers. Huu unakuwa ushindi wa pili mfululizo kwa klabu hiyo.

 

Rondo, mpaka sasa ametoa assist 22 katika michezo hiyo miwili, ameendelea kucheza dakika chache kutokana na uamuzi wa kocha ikisemekana ni katika utaratibu wa kuhakikisha anakuwa fiti. Rondo alicheza dakika 25 tu.

Taj Gibson alifunga pointi 12 huku akidaka rebound 8 na Robin Lopez akaongeza pointi 12 kwa upande wa Bulls.

Paul George na Myles Turner wote walifunga pointi 20 kwa upande wa Pacers (1-2), wakiwa wameshapoteza michezo miwili baada ya kuanza na ushindi, mchezo uliopita wakipoteza dhidi ya Brooklyn Nets.

HIGHLIGHTS

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here