Home Ligi EPL Kuondoka kwa Zlatan, PSG yapoteza mashabiki milioni 8

Kuondoka kwa Zlatan, PSG yapoteza mashabiki milioni 8

935
0
SHARE

zlatan-fans

Winger wa zamazni wa Manchester United Jesper Blomqvist amesema Paris Saint-Germain imepoteza mashabiki milioni nane baada ya Zlatan Ibrahimovic kujiunga na Mashetani Wekundu wa Premier League.

Ibrahimovic, 35, aliachana na mabingwa wa Ufaransa mwishoni mwa msimu uliopita baada ya misimu yake minne ya mafanikio akiwa Parc des Princes, pia mshambuliaji huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Sweden pamoja na Blomqvist wanaamini PSG imepoteza zaidi ya mchezaji.

“Ni mkiongozi mwa watu wenye heshimakubwa Sweden,” Blomqvist aliliambia The Sun. Amezindua perfume yake, magari aina ya Volvo pamoja na duka la vifaa vya michezo. Yeye tayari ni nembo kubwa ya kibiashara. Yupo kila mahali licha ya kwamba ameacha kucheza timu ya taifa.

“Ninafanya kazi nyingi na kampuni za usafirishaji za Sweden zinazokuja Manchester. Mahitaji ni zaidi ya mara tatu, Zlatan ni mtu mkubwa Sweden. Nadhani PSG wamepoteza mashabiki milioni nane kutoka Sweden ambao kwas asa wanaisupport Manchester United. Sio wote lakini ipo hivyo.

Plan nyingine zinakuja zaidi, wanauza ticket nyingi kwa mechi za United. Nimefanya hivyo kila mara kwa miaka kadhaa. Sasa kuna kampuni zaidi ya 10 zinazotaka niwapelekee mashabiki.

PSG wanapambana kutokana na kuondoka kwa Ibrahimovic kuanzia ndani ya uwanja hadi nje ya uwanja lakini kuondoka kwa mshambuliaji huyo kumekuwa kukihusishwa na mwanzo mbovu wa miamba hiyo ya soka la Ligue 1 chini ya kocha mpya Unai Emery.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here