Home Ligi EPL Liverpool ya Klopp haishikiki EPL baada ya kucheza mechi nane bila kupoteza

Liverpool ya Klopp haishikiki EPL baada ya kucheza mechi nane bila kupoteza

715
0
SHARE

1

Liverpool wamefanikiwa kuibuka na ushindi dhidi ya West Brom, lakini wameshindwa kulinda lango lango lao na kuruhusu bao moja lililowanyima nafasi ya kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi.

Vijana hao wa Jurgen klopp ambao walitawala mchezo huo walipata bao lao la kwanza kupitia kwa Sadio Mane kufuatia kazi nzuri ya Roberto Firmino.

Philippe Coutinho aliongeza bao la pili baada ya kupokea mpira mzuri kutoka kwa Sadio Mane na kuingia nao ndani na kumhadaa beki wa West Brom Gareth McAuley na kuuweka pembezoni kabisa wavuni.

Ushindi wa mabao mawili kwa bila ungewapeleka moja kwa moja kileleni lakini bao la dakika za mwisho za McAuley limezima ndoto hizo.

Lakini haikuishia hapo, ushindi huo umezidi kuwapa kiburi Liverpool baada ya kucheza mchezo wao wa nane bila kupoteza na kushika nafasi ya pili nyuma ya vinara Arsenal.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here