Home Kimataifa Huyu ndio Ronaldo Luiz Nazario De Lima Best Number 9 niliyemshuhudia

Huyu ndio Ronaldo Luiz Nazario De Lima Best Number 9 niliyemshuhudia

1362
0
SHARE

ronaldo_brazil_worldcup2002

Na Joel Chuku

Najua wengi wa kisasa  wamemshuhudia Di Lima ila wachache sana walimuelewa uwezo wake halisi wakati anacheza.

Wengi wetu enzi hizo tulikua tunamkubali kwakua tumekuta wakubwa zetu wanamkubali tu ila hatukua na akili hiyo ya kujua ubora wa mchezaji.

Ila kaa chini angalia documentaries zake (sio short videos za youtube) za huyo jamaa ndio utajua kua now days hamna namba tisa kama yake.

Nikimuangalia Suarez ambaye ndio namba tisa bora kwa sasa huyu jamaa anakipaji mno Suarez ila ukiwa makini utagundua Suarez huwa anajua mapema apeleke mpira wapi akiwa hata hajapewa huo mpira wenyewe.

Ni kama modern football ilivyo, Suarez ni master space na timing ukiongezea uwezo wake mkubwa basi anafunga tu mabao au kutengeza mnafasi za magoli  anakupa fundisho la kosa lako la position mbovu ukiwa kama defener.

Ronaldo De Lima alikua anajua sana kucheza na space na timing ila sio kwa ubora wa Suarez, De Lima ubora wake ulikua kwa vile hakua anazingatia sana mahali pa kuuweka mpira mapame huku akiwa bado hajaupokea bado.

Delima alikua anaupokea kwanza halafu ndio anatafuta pa kuupeleka au pa kufunga bila kujalia kama kuna mabeki wa kumkaba na huku akikuangalia defender unakuja kumzuia ila alikua haogopi kwakaua alikua anajua huwezi kumzuia na ulikua humzuii kweli.

Luis Suarez ukiangalia uchezaji wake hua  sio mtu wa kucommand mabeki sana kuliko  De Lima, kwakua Suarez yeye anatazama na weakness za mabeki na anaitumia weakness hiyo, Ronaldo De Lima alikua ana watengenezea hizo weakness hao mabeki.

De Lima alikua anafanya hivyo huku akiburuza mabeki, ana command mabeki wafate matakwa yake yeye na Mungu alimjalia move za hatari aisee hakua mchezaji wa direction moja au movement za haina moja alikua ana movement za kipekee sana.

Akiwa anaenda kushambulia jinsi anavyouweka mpira hakuoneshi kua atapitia upande wa kushoto wa kulia au atarudi nyuma alikua anaacha defender kwenye njia panda  sana.

Alikua ni kama mtu ambaye ni mmoja physically ila logically unaweza kuona kama watu wawili au watatu ambao wanashambulia kwa wakati mmoja, alikua ana miguu miwili kama vile ana miguu minne.

Huyu ndio Ronaldo Luiz Nazario De Lima Best Number 9 niliyemshuhudia na alikua nightmare kweli kwa mabeki.

Mfano rahisi kwa kumfananisha Ronaldo ni sawa na Mike Tyson yule wa mwaka 1988, Tyson wakati huo alikua anamdunda mtu huku akiwa anamfata kumpiga alikua hana muda wa kusubiri akiiingia kwenye ring anakufata anakutandika anachukua ushindi hakuwa na muda wa kumsikilizia mpinzani saaana.

Na ndio Ronaldo alivyokua hakua na muda wa kuwasoma sana mabeki position zao kwakua alikua anachukua mpira halafu ndio anaenda kuwashugulikia mabeki haijalishi mmejipanga vizuri au vibaya ila atapita tu kwakua alikua hazuiliki.

Nahisi uchezaji huo ndio maana hata mabeki wakawa wanamgeuza mboga kwa kumchezea rafu mbaya mno za kibabe kabisa  na kumsababishia asitimize ile potential yake aliokua nayo.

Kwa waliomuona Ronaldo akicheza sifa wanazo mpa na jinsi alivyokua anacheza vinaendana sawasawa kwakua zamani watu walikua wanaburudika na football zaidi kuliko kizazi hiki.

Ila kama umemsoma ronaldo kwenye google mafanikio yake kisoka ni sehemu ndogo tu uwezo wake halisi kiujumla aliokuwaga nao.

One hell of striker Ronaldo Luiz Nazario Delima fundi wa mpira.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here