Home Kimataifa  Mchezaji kushuka kiwango si sababu ya yeye kuzomewa

 Mchezaji kushuka kiwango si sababu ya yeye kuzomewa

623
0
SHARE

bood

Kushuka kwa kiwango cha mchezaji si sababu ya yeye kuzomewa, washabiki tumekuwa na tabia zisizo na aibu na naziita tabia za kinafiki kwa sababu humpenda sana mchezaji anapokuwa ‘ona fire’ na kosa tu aki-drop hata kidogo huanza kumkosoa na wengine kumpinga hata kujumuishwa katika timu zao za taifa ama katika vilabu vyao.

Inasikitisha sana kuona washabiki wanakuwa na tabia hizi najaribu kumuangalia mchezaji wa timu ya taifa ya England na klabu ya Manchester United Wayne Rooney ‘Wazza’ ni kweli Wazza kashuka kiwango lakini sio kama hawezi kutoa mchango wowote kwa timu yake ya taifa na klabu yake ya Manchester United.

Wakati Wazza akiwa on fire hakuna shabiki yeyote wa England na Manchester United alikua akimzomea Wazza ambaye ana jumla ya magori 53 zaidi ya mchezaji yeyote aliye wahi kuichezea timu ya taifa ya England na akiwa amefunga magoli 246 katika club yake ya Manchester United akiwa nyuma kwa magoli 3 tu kwa Bobby Charlton anaeshikilia rekodi yakuifungia United magoli mengi akiwa na jumla ya magoli 249.

Kwanini leo Wazza anapuuzwa na kuzomewa wakati akielekea mwishoni mwa soka lake? Kwanini asiheshimiwe kama walivyoheshimiwa wengine wakati wakielekea mwishoni mwa vipindi vyao vya soka? Si lazima kwa Wayne kuanza katika kikosi lakini apewe heshima yake klama naodha wa timu ya taifa ya England na club ya Manchester United.

Amalizie kipindi chake akiwa na raha kama wengine mbona kalitumikia taifa lake miaka mingi zaidi ya mchezaji yoyote aliyewai kuichezea timu ya taifa ya England, apewe heshima yake kama mchezaji mkongwe sasa kama washabiki ndio wa kwanza kumzomea itakuwaje kwa wachezaji anaowaongoza? Ata sema nini kama kiongozi?

Hizi tabia za kinafiki tuziache na nimeingalia Ufaransa pia wamepiga sana kelele Paul Pogba aachwe kwenye kikosi maana kashuka kiwango lakini ndiye aliyeifungia goli pekee timu yake ya taifa ya Ufaransa dhidi ya Uholanzi, haohao waliokuw wakimpinga hawakusita kulishangilia goli hilo sasa kwanini wasingeendelea kupinga hadi goli alilofunga maana hana kiwango cha kuwa kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo ya ufaransa.

Namna waingereza walivyo wanafiki wakati Sam Allardyce ametwaa kikosi hicho cha Three lions aliwaita wachezaji kama Dier, Henderson, Lallana, Rooney, Sterling baadhi ya washabiki walituma tweets na kuanza kusema  Allardyce ni kama Roy kwa sababu kamuacha Danny Drinkwater  kawatumia hao wachezaji walioshindwa kufanya vizuri Euro sasa leo tena wanamtaka Dier na hawamtaki Rooney, wamempenda Henderson aliekuwa chini ya kiwango wakati wa Euro na sasa karejea kwenye kiwango cha bora kabisa wanaanza unafiki wakuonesha kumpenda tena?

Hivyo hivyo kwa Theo Walcott pia alipita katika kipindi hichohicho kigumu cha kuonekana kachoka hafai tena lakini sasa karejea tena kawa lulu kama zamani? Na huyo Wayne ndio anapitia pia kipindi hicho kwa sasa na ninaamini atarejea na atamaliza kipindi chake cha soka akiwa vizuri na atapewa heshima na hao mashabiki wanafiki

Ipo siku Wayne atarejea tena katika kiwango chake bora  wataanza tena kumshabikia hii sio tabia ya soka kabisa tujaribu kuiga mifano ya wajerumani huthamini wachezaji ndio maana taifa lao linafika mbali hawakuacha kumshangilia na kumuaga kwa makofi na upendo wa hali ya juu Bastian Schweinsteiger japo kocha wa Manchester United José Mourinho aliamua kuacha kumjumuisha katika kikosi chake lakini wajerumani bado walimkubali sana ‘teiger’.

Pia walionesha upendo kwa Miroslav Klose licha yakuwa na umri mkubwa wa miaka 36 lakini walitamani avunje rekodi japo walikuwa na makinda wengi wadogo na wenye uwezo mkubwa lakini hawakumuacha nyuma Miroslav Klose lakini leo Wayne mwenye umri wa miaka 30?

Natupa jiko kwa mashabiki wa Ufaransa na baadhi pia wanashindwa kuutambua mchjango wa Olivier Giroud mwenye magori 21 akiwa nafasi ya 11 kwa wafungaji wa Ufaransa na bado anakitu cha kuifanyia Ufaransa tujaribu kuutafsiri na kuuelewa msemo unaosema ‘ukipata kipya cha zamani usikisahau’ England mmepata vitu vipya ndio lakina hata vya zamani pia ni lulu hivyo vipya pia itafika wakati mtavizomea, jaribuni kushikamana kuonesha mapenzi kwa wachezaji wenu ili wazidi kuwatumikia vizuri na kwa weledi katika timu, zenu mnapowazomea na kuwaona hawafai mnawakatisha tamaa.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here