Home Kimataifa Courtois ‘amwakia’ Hazard Ubelgiji

Courtois ‘amwakia’ Hazard Ubelgiji

603
0
SHARE

1Thibaut Courtois alichukizwa na kitendo cha mchezaji mwenza wa Chelsea Eden Hazard kufanya masihara ambayo yangepelekea kuruhusu goli na kuharibu clean sheet katika mchezo ambao Ubelgiji walishinda mabao 6-0 dhidi ya Gibraltar.

Katika mchezo huo, Benteke alifunga goli la mapema kabisa mnamo sekunde ya saba kabla ya kuhitimisha hat-trick yake baadae katika mchezo huo.

Hata hivyo Courtois hakupenda kile alichokifanya Hazard, ambaye alifunga goli la sita na kusema kwamba mchezaji mwenza huyo wa Chelsea angeweza kusababisha timu yao kuruhusu bao kutokana na manjonjo yake yasiyo ya lazima.

“Nilikuwa na hasira kwa kitendo alichofanya Hazard kwasababu alijaribu kupiga kwa kisigino katika eneo ambalo halikuwa sahihi,” alisema.

“Nia yangu kubwa ilikuwa ni kupata clean sheet. Nilitaka kila mmoja afahamu hilo kwamba tulipaswa kuwa makini mno.

“Tulioenesha kuwaheshimu sana wapinzani wetu. Bado tuna kama mwaka mmoja na nusu hivi kuthibitisha ubora wetu kama tuko tayari kupambana kuwania Kombe la Dunia.”

Mpaka sasa Ubelgiji ndio vinara wa Kundi H wakiwa na alama tisa baada ya kucheza michezo mitatu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here