Home Dauda TV Video: Ronaldo alivyofurahia selfie na shabiki

Video: Ronaldo alivyofurahia selfie na shabiki

640
0
SHARE

ronaldo-selfie

Kabla ya kipindi cha pili kuanza mchezo kati ya Faroe Islands na Ureno, shabiki alikimbia na kuingia uwanjani akitaka kupiga picha (selfie) na star wa Real Madrid Cristiano Ronaldo katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2018.

Ronaldo hakukataa, alipiga picha na shabiki huyo.

Ureno iliiangamiza Faroe Islands 6-0 ugenini kwenye mchezo wa kuwania kufuzu michuano ya Kombe la Dunia 2018.

Hat-trick kutoka kwa striker wa Porto kijana mwenye miaka 20 Adre Silva kwenye kipindi cha kwanza iliiweka Ureno kwenye nafasi nzuri ikiwa kwenye mechi ya ugenini.

Ronaldo alifunga goli la nne akiwa nje kidogo ya eneo la penati box akipiga shuti kwenye kona ya juu na kuihakikishia Ureno ushindi kwenye mchezo wao wa ugenini.

Waliongeza magoli mengine mawili wakati wa dakika za lala salama kukamilisha ushindi wa magoli 6-0.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here