Home Dauda TV Video: Goli la Pogba la mita 30 lilivyoipa ushindi Ufaransa dhidi ya...

Video: Goli la Pogba la mita 30 lilivyoipa ushindi Ufaransa dhidi ya Uholanzi

869
0
SHARE

paul-pogba-strike

Tayari yalishaanza maneno kwa kocha wa Ufaransa Didier Deschamps kwamba ampige chini kiungo wa Manchester United Paul Pogba kwenye kikosi cha Ufaransa kilichocheza dhidi ya Uholanzi.

Nyota huyo mwenye miaka 23 amelipa fadhila za kuaminiwa na kocha wake baada ya kufunga goli pekee kwenye mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2018 dhidi ya Uholanzi

Akiwa umbali wa zaidi ya mita 30 kutoka golini, Paul Pogba aliachia shuti kali ambalo lilimshinda golikipa wa Everton Maarten Stekelenburg licha ya kujaribu kupangua shuti hilo.

Golikipa huyo mdachi alipambana kadri alivyoweza ili kuzuia shuti la Pogba lakini hakuweza kufanya kile ambacho alitarajia kukifanya na hatimaye kuzishuhudia nyavu zake zikicheza.

Sasa huenda mashabiki wa Manchester United wakawa na matumaini mapya ya kumuona Pagba akifunga magoli mengine kama hayo akiwa kwenye klabu yake ya Old Trafford.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here