Home Kimataifa Balotelli: Simfahamu kiumbe anayeitwa Klopp

Balotelli: Simfahamu kiumbe anayeitwa Klopp

1009
0
SHARE

1Mario Balotelli amefichua kwamba hakuwa na uhusiano wowote na Jurgen Klopp, ambaye alimwambia mchezaji huyo kuondoka Liverpool kwa mkopo.

Muitaliano huyo alisajiliwa na Brendan Rodgers mwaka 2015 kutoka AC Milan, lakini alishindwa kabisa kuonesha makali yake kabla ya kurudi tena AC Milan kwa mkopo.

Kwa sasa anakipiga kunako klabu ya Nice, ambapo tayari ameshafunga mabao sita kwenye michezo mitano baada ya kuondoka Liverpool bure kwenye dirisha la usajili la majira ya kiangazi.

Na sasa Balotell amefichua kwa kusema kwamba hapakuwa na uwezekano wowote kwake kurudi Anfield kutokana na uhusiano usioridhisha kati yake na Klopp.

“Klopp? Simjui mimi huyo mtu,” Balotelli aliiambia Sky Sport Italia. “Aliniambia tu niondoke Liverpool kwa mkopo na baadaye nikarejea kumwambia: ‘Asante sana, na kwaheri.'”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here