Home Kimataifa Video: Kama ulidhani Balotelli ametulia ulikosea, afanya balaa Ufaransa

Video: Kama ulidhani Balotelli ametulia ulikosea, afanya balaa Ufaransa

1027
0
SHARE

mario-balotelli

Mario Balotelli kwa sasa anawafunga midomo wote waliokuwa wanasema amekwisha.

Muitaliano huyo alikuwa kwenye wakati mgumu wakati wa majira ya usajili wa dirisha la kiangazi kutokana na timu nyingi za ligi kubwa za Ulaya kuonesha hazivutiwi nae hadi mwishowe Nice walipoamua kujitosa kumchukua kama wanacheza bahati nasibu.

Hadi sasa Balotelli amewalipa kwani tayari ameshafunga magoli 6 kwenye mechi 6, huku goli lake la sita akifunga dakika za lala salama wakati timu yake ikipata ushindi dhidi ya Lorient.

Lakini Balotelli anabaki kuwa Balotelli tu, amejikuta analambwa kadi nyekundu baada ya kugombana na mchezaji wa Lorient.

Awali alioneshwa kadi ya njano baada ya kushangilia goli lake kwa kuvua jezi kisha akaoneshwa kadi ya pili ya njano muda  mfupi kutokana na tukio la kuoneshana ubabe na mchezaji wa Lorient ambapo anaonekana kama alimpiga kichwa licha ya tukio hilo kuonekana kama ni jepesi ukilinganisha na adhabu.

Goli alilofunga Mario Balotelli dhidi ya Lorient

Balotelli anaoneshwa kadi nyekundu

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here