Home Kitaifa Audio: Jamhuri Kihwelu ‘Julio’ atangaza kuachana na soka

Audio: Jamhuri Kihwelu ‘Julio’ atangaza kuachana na soka

665
0
SHARE

dsc_0247

Kocha mkuu wa Mwadui FC Jamhuri Kihwelu ‘Julio’ ametangaza rasmi kuacha kufundisha soka la Tanzania kutokana na maamuzi mabovu katika baadhi ya michezo ligi kuu Tanzania bara.

“Kuanzia leo na kuendelea, sitaki tena mpira. Najiuzulu mpira moja kwa moja sitaki kwasababu mpira wa Tanzania unachezwa kwa siasa sana. Mpira unachezwa kwa ajili ya kufurahisha watu hata wasiokuwa na uwezo waonekane wanajua, hiki kitu kinaumiza sana”, amesema Julio baada ya mchezo kati ya Mbeya City vs Mwadui uliomalizika kwa vijana wa Julio kulala kwa bao 1-0 ugenini.

“Nimeshafundisha mpira Qatar, Yemen na Dubai lakini sijawahi kufeli lakini kuna kundi la watu wanajua huyu ukimfanyia hivi unamharibia ni kuharibu mpira wetu ndio maana vilabu vyetu vikienda kwenye mashindano ya kimataifa havifanyi vizuri.”

“Kwahiyo kuanzia sasahivi natangaza sitaki kuwa kocha wa mpira wa Tanzania tena labda nikipenda niwe naenda kuangalia mpira lakini kinyume cha hapo sitaki mpira kwasababu tunakoelekea siko. Kuna watu watasikitika kutoka kwangu kwenye mpira lakini kwa kipindi hiki bora nipumzike nifanye kazi nyingine kwanza, mawashuru watanzania wote waliokuwa karibu na Julio.”

Unaweza kusikiliza sauti hapa chini Julio alivyoamua kutangaza kuacha kufundisha soka la Tanzania

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here