Home Ligi EPL Nje ya pitch- Mourinho anaongea navajo kuhusu Rooney

Nje ya pitch- Mourinho anaongea navajo kuhusu Rooney

824
0
SHARE

Mou-China

Na Athumani Adam

Navajo ni jamii ya kihindi ambayo inapatikana Kusini mwa Marerkani. Kwenye jimbo la Utah wanakadaliwa kufika watu milioni 3 kutokana na sensa ya mwaka 2015. Pia wanapatikana Arizona na Mexico.

Inasemekana jeshi la Marekani kwenye vita ya pili ya dunia walitumia lugha ya jamii hii ili kuweka ugumu kwa maadui kutojua mbinu za jeshi lao endapo mawasiliano yatadukuliwa.

Baada ya miaka kadhaa kupita tangu Navajo kutumika kwenye vita ya pili, Jose Mourinho wiki iliyopita alikuwa bize kuongea Navajo kwenye soka. Baada ya mechi ya kombe la Ligi, habari kubwa ilikuwa ni kiwango duni cha naodha wake Wayne Rooney.

Mourinho alitumia kila aina ya maneno kumlinda Rooney dhidi ya shutuma za kushuka kiwango.  Aliweza kutumia weledi kumlinda Rooney, hakutaka kurudia kosa ambalo alilifanya akiwa na Madrid ambapo aliwahi kumsema Iker Casillas hadharani. Aliongelea zaidi kuhusu timu kuliko mchezaji mmoja Rooney.

Lakini kwa upande wa pili, kile kilichofanywa na Mourinho kwenye mchezo dhidi ya Leicester ligi kuu England siku ya Jumamosi ni wazi kwamba Mourinho amemsema Rooney kwa vitendo.

Kitendo cha kutomuanzisha Rooney kwenye kikosi cha kwanza pamoja na wachezaji kadhaa ambao wamezoeleka kuonekana kwenye kikosi cha kwanza tangu mwanzoni mwa msimu kuliifanya Man Utd kuwa bora.

Juan Mata alipata fusra kucheza eneo analolipenda, nyuma ya mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic.  Mata hatumii nguvu sana kama Rooney, lakini uwezo wa kufikiri kwa haraka, kasi pamoja na maamuzi sahihi akiwa uwanjani ulichangia kucheza vizuri na kuleta faida kubwa kwa timu yake.

Ander Herrera alianza badala ya Felaini jambo ambalo lilichangia kwa kiasi kikubwa Paul Pogba kucheza kwa uhuru zaidi kwa ile staili ya box to box bila kusahau kasi ya Rashford na Lingard kutokea pembeni

Bahati mbaya eneo alilocheza Mata  linashikiliwa na nguli Rooney kwa miaka mingi sasa. Awe kwenye ubora au kiwango duni makocha wote wamemfanya Rooney ndiye mfamle pekee ambaye anaweza kucheza nyuma ya mshambuliaji.

Makocha ambao wamepita Man Utd hawathubutu kumuweka Rooney benchi bila ya kuwa na tatizo lolote la kiafya. Kina Shinji kagawa wameshindwa kuwika ndani ya Old Trafford sababu ya Mfamle Rooney.

Hata msimu uliopita japokuwa hakuwa bora sana hadi kufika mwezi Desemba ambapo alipata majeraha bado kocha Van Gaal aliendelea kumuamini Rooney licha ya kuwa kwenye kiwango duni. Yawezekana ufamle huu unatokana na utamaduni wa Man Utd kutumia washambuliaji wawili kwa wakati mmoja.

Huu ni utamaduni wa muda mrefu sana pale Old Trafford kuanzia enzi za Eric Cantona na Mark Hughes.

Hata alichokifanya Mourinho juzi ni kumpa muda Rooney wa kujirekebisha ili aweze kurudi kwenye kiwango chake.  Ukisikiliza interview baada ya mechi ya Leicester kuiisha anaendelea kukiri kuwa Rooney ni mchezaji bora, anaendelea kutumia Navajo kumjenga tena Wyne Rooney.

Sina hakika na maamuzi yajayo ya Mourinho endapo Rooney akishindwa kuerejea kwenye kiwango.  Mwezi October Rooney atakuwa anasherekea Birthday yake ya thelathini na moja, sijui kama anaweza kuleta kitu kipya ndani ya United. Tusubiri tuone

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here