Home Kitaifa Picha: Yanga walivyokamilisha mazoezi yao kabla ya kuikabili Stand United

Picha: Yanga walivyokamilisha mazoezi yao kabla ya kuikabili Stand United

888
0
SHARE

dsc_0034

Kikosi cha Yanga chini ya benchi la ufundi linaloongozwa na kocha Hans van der Pluijm kimefanya mazoezi yake ya mwisho kwenye uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga tayari kupambana na Stand United kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara.

dsc_0069

Wachezaji wote waliosafiri na timu wamefanya mazoezi na hiyo inaashiria kikosi kizima kipo tayari kwa ajili ya mchezo dhidi ya Wakali wa Shinyanga mjini.

dsc_0061

Yanga imecheza mechi 5 imefunga magoli 8 huku ikiwa bado haijafungwa goli hata moja.

dsc_0044

Kwa upande wa Stand United nao hawajapoteza mchezo katika michezo yao mitano iliyopita. wamepata sare tatu na kushinda mechi mbili. Mechi zote walizoshinda ni zile walizocheza kwenye uwanja wao wa nyumbani.

dsc_0088

Mechi ya mwisho Yanga wameshinda 2-0 dhidi ya Mwadui FC ambao ni wapinzani wakubwa wa Stand United.

dsc_0072

Stand United nao walishinda 2-1 mchezo wao wa mwisho dhidi ya JKT Ruvu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here