Home Kimataifa ICARDI, PERISIC, WAVUNJA REKODI YA JUVE SERIE A 

ICARDI, PERISIC, WAVUNJA REKODI YA JUVE SERIE A 

744
0
SHARE

1

Inter Milan walitoka nyuma na kuwatandika Juventus katika mchezo mkali na wa kusisimua wa derby d’Italia.

Stephan Lichtsteiner aliwapa Juve goli la uongozi dakika ya 66 baada ya kuunganisha krosi nzuri kutoka kwa Alex Sandro.

Hata hivyo, baadaye Mauro Icardi aliswazisha bai kwa wenyeji wa mchezo huo Inter Milan dakika mbili baadaye kwa kuunganisha kwa umahiri mkubwa mpira wa kona.

Ivan Perisic, ambaye aliingia akitokea benchi aliwapa Inter bao la pili kufuatia kazi nzuri iliyofanywa na Icardi, and Juve, huku Gonzalo Higuain ambaye pia aliingia kutokea bechi akishindwa kufurukuta ili kuisawazishia timu yake bao

Mchezaji wa Inter Milan Ever Banega alipewa kadi nyekundu dakika ya tisini.

Matokeo hayo yanafanya Juve kupoteza mchezo wake kwa mara pili kwenye Serie A tangu walivyofungwa bao 1-0 na Sassuolo 28 October, 2015.

Kipigo hicho pia kinamaanisha kwamba Mabingwa Watetezi hao wanashuka mpaka nafasi ya pili nyuma ya Napoli, wakati Inter wakijisogeza mpaka nafasi ya sita.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here