Home Ligi EPL GUARDIOLA: DE BRUYNE NI WA PILI KWA UBORA BAADA YA MESSI

GUARDIOLA: DE BRUYNE NI WA PILI KWA UBORA BAADA YA MESSI

928
0
SHARE

1Pep Gurdiola amemuelezea Kevin De Bruyne kama moja ya wachezaji bora ambao amewahi kuwafundisha.

De Bruyne alifungua ukurasa wa mabao kwa Man City jana kwa mkwaju mkali uliotokana na mpira wa kutenga na kuchangia ushindi wa mabao 4-0 ambao timu yake uliupata dhidi ya Bournemouth katika mchezo wa Premier League uliochezwa kwenye Uwanja wa ;Etihad Stadium.

Guardiola amewafundsha wachezaji wengi wenye majina makubwa kama vile Arjen Robben, Andres Iniesta na Xavi.

Na tayari ameshasema kwamba katika wachezaji wote aliowahi kuwafundisha katika nykati tofauti, nyota wa Barcelona Lionel Messi ndiye bora kuliko wote, lakini sasa hivi amekuja na mpya tena baada ya kusema kwamba De Bruyne ndiye anayefuata baada ya Messi.

“Ni moja ya wachezaji bora sana ambao nimewahi kufanya nao kazi,” kocha huyo wa zamani wa Barcelona na Bayern Munich alisema. “Messi yuko kwenye meza ya tofauti, lakini Kevin yuko meza inayofuata na yuko sahihi sehemu alipo.”

“Ni mchezaji mwenye uwezo wa kuusoma mchezo kwa haraka zaidi, mwili wake uko imara pia,” Guardiola ameongeza.

“Ni mpiganaji asipokuwa na mpira lakini vilevile zaidi akiwa na mpira, ni ukweli ulio wazi kwamba anaona kila kitu awapo uwanjani. Na awapo mbele ya goli anaweza kupiga pasi hatari na kufunga pia. Tuna bahati kubwa ya kuwa na Kevin.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here