Home Kitaifa NAHITAJI MTAJI MBEYA CITY VS PRISONS – JEREMIA JUMA

NAHITAJI MTAJI MBEYA CITY VS PRISONS – JEREMIA JUMA

630
0
SHARE

jeremia-prison-20160914_072650

Mshambuliaji wa kikosi cha maafande wa Magereza Jeremia Juma amesema anahitaji kufunga katika mechi ya Mbeya derby inayopigwa leo jiioni (Jumamosi September 17) kwenye uwanja wa Sokoine, Mbeya. Jeremia amesema lengo lake ni kufunga katika mchezo huo ili kujiweka katika nafasi nzuri ya orodha ya wafungaji wa VPL msimu huu.

Mfungaji huyo wa Prisons tayari ameshafunga goli moja msimu huu akizidiwa magoli mawili na Laudit Mavugo na John Bocco wanaoongoza rodha ya wafungaji baada ya mechi nne zilizopita.

“Ni mechi muhimu kwangu, nahitaji kufunga ili nijiongezee magoli nikiwa kama mshambuliaji. Mfungaji anayeongeza anamagoli matu mimi tayari nimefunga moja, kwahiyo nahitaji kufunga ili kujiweka kwenye nafasi nzuri kwenye orodha ya wafungaji”, anasema askari magereza Jeremia Juma aliyefunga magoli 15 VPL msimu uliopita lakini TFF ikiwa ilimpa magoli 11.

“Tumejipanga vizuri licha ya kuwepo na upinzani mkali katika mechi hii kuanzia nje ya uwanja hadi ndani ya uwanja. Hakuna kingine tunachohitaji zaidi ya pointi tatu”, anasema Jeremia ambaye amefunga goli moja tangu ameanza kucheza dhidi ya Mbeya City akiwa TZ Prisons.

Tanzania Prisons wanajivunia matokeo ya mechi mbili za msimu uliopita dhidi ya City, katika game ya kwanza ‘wajelajela’ walilazimisha sulusu na kupata ushindi wa goli 1-0 katika game ya raundi ya pili.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here