Home Kitaifa MBEYA CITY FC VS TANZANIA PRISONS: ‘DERBY’ YA MBEYA INAYOPIGWA JUMAMOSI HII

MBEYA CITY FC VS TANZANIA PRISONS: ‘DERBY’ YA MBEYA INAYOPIGWA JUMAMOSI HII

1038
0
SHARE

mbeya-city-vs-prisons

Na Baraka Mbolembole

ACHANA na moja ya ‘derby’ za Dar es Salaam ambazo zitawakutanisha ‘wababe wa ligi’ Azam FC vs Simba SC au ‘derby’ ya kwanza ya msimu huu katika VPL iliyopendezeshwa na magoli manne ya kipindi cha kwanza kati ya Mwadui FC 2-2 Stand United.

Siku ya Jumamosi ijayo timu hasimu za jiji la Mbeya, Mbeya City FC na Tanzania Prisons zitavaana katika raundi ya tano ya ligi kuu Tanzania Bara.

Hli ni ‘pambano lingine la wiki.’ Hili litakuwa pambano la 7 kwa timu hizi kukutana katika VPL. City iliwachapa TP katika game zote mbili msimu wa 2013/14 ambao ulikuwa ni wa kwanza katika VPL kwa timu hiyo ya ‘Kizazi Kipya.’

Historia ya mipambano 6 iliyopita

Peter Mapunda ndiye mchezaji wa kwanza kufunga goli katika pambano la City v Prisons. Ilikuwa katika pambano ambalo City walishinda 2-0 (magoli ya Mapunda na Deo Julius) katika game ya kwanza msimu wa 2013/14. Prisons wakalazwa 1-0 katika mechi ya mzunguko wa pili kwa goli la Paul Nonga.

Michezo 6 ya mwisho baina ya timu hizo kila timu imefanikiwa kushinda mara mbili na game mbili zilimalizika kwa sare. Baada ya City kushinda game zote mbili msimu wa 2013/14 mambo yakageuka msimu uliofuata.

Mechi ya raundi ya kwanza ilimalizika kwa sare ya timu hizo kufungana 2-2 na game ya raundi ya pili Prisons ilishinda kwa mara ya kwanza kwa msaada wa goli la mkwaju wa penalti lililofungwa na mlinzi wa kati, Lugano Mwangama.

Hiyo ilikuwa msimu wa 2014/15 na msimu uliopita Prisons ilifanikiwa kushinda 1-0 katika game ya raundi ya pili huku ile ya kwanza ikimalizika kwa suluhu-tasa.

Vikosi vinavyotaraji kupambana jumamosi hii 

City wapo nafasi ya nne wakiwa na alama 7 sawa na Prisons walio nafasi ya tano. City wamefanikiwa kufunga magoli 6 na kuruhusu nyavu zao mara tatu wakati Prisons imefanikiwa kufunga magoli matatu tu na kuruhusu mawili golini mwao.

Timu zote zina makocha wataalam, Meja Mstaafu, Mingange ambaye alikuwa kocha City msimu uliopita lakini alitimuliwa na kumpisha Mmalawi, Kinnah Phiri. Wawili hao watakutana kwa mara ya kwanza Jumamosi hii.

Phiri atakuwa na Wamalawi watatu katika kikosi chake cha kwanza, golikipa Owen atasaidiwa na wazawa Haruna Shamte, Hassan Mwasapili katika beki za pembembeni. Kijana Rajab Zahir na raia mwingine wa Malawi katika beki ya kati.

Ken Mwambungu, Ramadhani Chombo, kiungo Mmalawi na Joseph Mahundi wanataraji kukamata kiungo cha City na kuwalisha washambuliaji Raphael Alpha na Ditram Nchimbi ambao tayari wamefunga jumla ya magoli matatu kwa pamoja.

Mingange yeye hatakuwa na mchezaji yeyote wa kigeni katika timu yake. Andrew Ntala, Michael Ismail, nahodha, Laurian Mpalile, James Mwasote na Nurdin Chona wataunda safu ya ulinzi. Jumanne Elfadhili, Lambert, Mohamed Samatta na Leons wanataraji kuanza katika safu ya kiungo na mbele kabisa safu ya mashambulizi, wanataraji kupangwa, Victor na Jeremiah Juma.

Nani mshindi wa game hii?

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here