Home Ligi EPL KLOPP AWEKA REKODI MPYA EPL, LIVERPOOL IKIIADHIBU CHELSEA 2-1 DARAJANI

KLOPP AWEKA REKODI MPYA EPL, LIVERPOOL IKIIADHIBU CHELSEA 2-1 DARAJANI

1015
0
SHARE

1Antonio Conte amepata kipigo chake cha mara ya kwanza akiwa kama bosi wa Chelsea baada ya Liverpool kuwafunga Darajani kwa mabao 2-1 na kuchupa moja kwa moja mpaka nafasi ya nne wakiwa na alama 10 sambamba na Chelsea lakini wakizidiwa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa.

Beki wa kati wa Liverpool Dejan Lovren aliifunga goli la kwanza baada ya kuuganisha krosi kutoka kwa Philippe Coutinho kutokana na mabeki wa Chelsea kuchelewa kumkaba.

Jordan Henderson, ambaye ni nahodha wa Liverpoo akaongeza la pili baada ya kuachia shuti kali ( thunderbolt) na kwenda mapumziko wakiwa na akiba ya mabao mawili mkononi.

Kipindi cha pili Chelsea waliimarika na kupata bao kupitia kwa Diego Costa ambaye aliunganisha pasi ya Nemanja Matic, lakini mpaka mwisho wa mchezo matokeo yalibaki kuwa hivyohivyo.

Liverpool wamefikisha alama 10 sambamba na Chelsea na Everton.

Vijana hao wa Jurgen Klopp pia wameshawaadhibu Arsenal na Mabingwa Watetezi Leicester,jumlisha droo dhidi ya Tottenham, huku wakipoteza mchezo mmoja tu dhidi ya timu iliyopanda daraja msimu huu ya Burnley.

Dondoo muhimu

 • Liverpool wameshinda mechi tano kati ya tisa zilizopita walizocheza Stamford Bridge.
 • Antonio Conte amepoteza mchezo wake wa kwanza wa nyumbani akiwa kama kocha tangu Januari 2013, akihitimisha mfululizo wa michezo 30 bila kupoteza
 • Tangu Klopp achukue mikoba ya kuinoa Liverpool wamefunga mabao 15 nje ya boksi, magoli matano zaidi ya timu yoyote.
 • Diego Costa amehusika walau katika goli moja kwenye kila mchezo aliocheza mpaka sasa katika msimu huu wa ligi (magoli matano, pasi ya goli moja).
 • Ni Sergio Aguero pekee ndiye mchezaji mwenye magoli mengi kwenye Premier League mwaka 2016 kuliko Costa (magoli 18 na assists sita).
 • Dejan Lovren amemaliza ukame wa kucheza mechi 64 bila ya kufunga kwenye Ligi ya England, mara ya mwisho alifunga dhidi ya Sunderland mwaka 2014 wakati huo akicheza Southampton.
 • Chelsea wamekosa clean sheet katika mchezo wowote kati ya saba iliyopita dhidi ya Liverpool, mara ya mwisho ilikuwa ni Oktoba mwaka 2009.
 • Kwa mara ya kwanza tangu Desemba 2015, Chelsea wamekuwa nyuma kwa mabao mawili kwenye mchezo wa Premier League katika kipindi cha kwanza. Mara ya mwisho ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya Leicester, mchezo ambao ulikuwa wa mwisho kwa Mourinho.
 • Nemanja Matic ametoa assist kwenye kila mchezo kati ya miwili iliyopita ya Premier League katika Uwanja wa Stamford Bridge, mara nyingi zaidi kuliko alivyofanya kwenye michezo 38 iliyopita waliyocheza nyumbani.
 • Liverpool wamekosa clean sheet kwenye michezo tisa ya ugenini ya Premier League. Mwenendo mrefu zaidi tangu May 2005.
 • Jurgen Klopp ni meneja wa kwanza kushinda mfululizo michezo yake miwili ya mwanza aliyocheza Stamford Bridge kwenye Premier League tangu mara ya mwisho alivyofanya hivyo Arsene Wenger, na meneja wa nne kwa ujumla kufanya hivyo mbali na Mike Walker na Harry Redknapp.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here