Home Kimataifa DIEGO SIMEONE AAMUA KUIKACHA ATLETICO MADRID

DIEGO SIMEONE AAMUA KUIKACHA ATLETICO MADRID

510
0
SHARE
MADRID, SPAIN - JANUARY 07: Head coach Diego Pablo Simeone of Atletico de Madrid encourages his team during the Copa del Rey Round of 16  first leg match between Club Atletico de Madrid and Real Madrid CF at Vicente Calderon Stadium on January 7, 2015 in Madrid, Spain.  (Photo by Gonzalo Arroyo Moreno/Getty Images)

Kocha wa klabu ya Atletico Madrid Diego Simeone “El Cholo” hatimaye siku ya leo amethibitisha taarifa zilizokuwa zimezagaa kuwa ni kweli amepunguza mkataba wake wa kuitumikia na kuifundisha klabu hiyo ya nchini Hispania.

Mkataba wake wa awali ambao alisaini kipindi cha mwezi March mwaka 2015 ulipangwa kumalizika kipindi cha msimu wa mwaka 2020. Kwa maana hiyo kutokana na maamuzi yake ya kuamua kupunguza miaka miwili, sasa maana yake ni kuwa utakoma katika msimu wa mwaka 2018.

Diego Simeone”El Cholo”, 46, pamoja na kuulizwa kwa undani sababu za yeye kufikia maamuzi hayo bado alisita kuweka wazi sababu zilizopelekea yeye kuamua kufikia maamuzi hayo ambayo hayakutegemewa katika siku za karibuni, ingawa ameweka wazi tu kuwa pande zote mbili zimefikia makubaliano ambayo ni sahihi na yenye manufaa kwa wote.

Aidha kocha huyo ambaye ni raia wa Argentina hakuficha hisia zake kuwa siiku zote amekuwa ni mwenye furaha kuwa na klabu ya Atletico Madrid na ataendelea kuwa na furaha katika miaka miwili iliyobaki na akatania kuwa anaweza akasaini mkataba mpya.

Simeone alianza kuifundisha klabu hiyo mwisho mwa msimu wa mwaka 2011, na kufanikiwa kuiwezesha kuchukua taji la liguu ya Hispania, La Liga mara moja (2014), kombe la mfalme (2013) na wakifanikiwa kuingia fainali ya klabu bingwa ulaya mara 2, zote wakifungwa na jirani zao na wapinzani wao wakuu yaani klabu ya Real Madrid.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here