Home Kitaifa Exclusive: Kwanini Telela aliikacha Simba na kuamua kusaini Ndanda FC?

Exclusive: Kwanini Telela aliikacha Simba na kuamua kusaini Ndanda FC?

903
0
SHARE

img_0028

Kuna maswali mengi ambayo yamekuwa haya majibu kwa mashabiki wengi wa soka nchini kufatia kuwepo na uvumi kwamba, kiungo wa zamani wa Yanga Salum Telela anayekipiga Ndanda alitaka kusajiliwa na Simba lakini mambo yakashindikana.

Swali ambalo linaibuka hapa ni kwamba, kwanini Simba walishindwa kumsajili Telela hadi akaibukia Mtwara?

shaffihdauda.co.tz iliamua kumtafuta Telela ili kujibu swali hilo, Telela ameeleza sababu ya kushindwa kukipiga kwa ‘Wekundu wa Msimbazi’ licha ya kutotoboa kabisa jipu, lakini kwa alichokieleza nadhani wewe msomaji utaelewa vizuri pia.

shaffihdauda.co.tz: Kwanini ulichagua kwenda Ndanda?

Telela: Sababu ya msingi ni kwamba, mimi nimeamua kurudi tena shule, Mtwara ndipo kilipo chuo ambacho mimi nasoma kwahiyo nisingeweza kwenda kucheza timu nyingine nje ya Mtwara zaidi ya Ndanda. Ningeenda nje ya Mtwara nisingeweza kusoma, kwahiyo kuwepo hapa ni sababu ya ujirani na shule ili niweze kufanya mambo yangu ya kishule kwa urahisi zaidi.

shaffihdauda.co.tz: Kuna taarifa zilienea kwamba, Simba walikufata baada ya mkataba wako na Yanga kumalizika, je ni kweli? Na kwanini haukujiunga na Simba ukaenda Ndanda?

Telela: Simba walikuja tukakaa tukazungumza lakini hawakufikia matakwa yangu, lakini kama wangetekeleza vitu ambavyo nilikuwa nataka ningecheza Simba. Na sio Simba pekeake mimi nacheza popote pale iwapo tutafikia makubaliano.

shaffihdauda.co.tz: Wakati upo Yanga ulikuwa unakutana na changamoto gani?

Telela: Kucheza Yanga ni tofauti na hivi vilabu vingine vidogo. Yanga imezungukwa na watu wengi, changamoto zipo kutoka kwa mashabiki, viongozi hadi wachezaji kwasababu unakuta unalipwa hela nyingi.

shaffihdauda.co.tz: Baada ya mkataba wako kumalizika Yanga na hawakuonesha nia ya kutaka kuendelea na wewe. Familia walichukuliaje hili?

Telela: Mimi ni damu yao, familia haiwezi kukata tamaa kwa hilo, hii ni moja ya changamoto za maisha. Mimi sikuzaliwa nikiwa najua nitacheza Yanga kwa muda wote. Kikubwa ilichofaya familia yangu ni kukaa chini na mimi na kujadili tukajua tufanyaje. Hawakusikitishwa sana na hilo badala yake wakanipa moyo kwa nilichopitia.

shaffihdauda.co.tz: Unadhani ni kitu gani kilisababisha Yanga wasikuongezee mkataba mwingine wa kuendelea kubaki Jangwani?

Telela: Kwa hilo mimi sijajua, ni uongozi au sababu za kiufundi. Wao hawakuwa tayari kukaa na mimi kuzungumzia mkataba mpya. Kwahiyo nadhani sababu watakuwa wanayo wenyewe.

shaffihdauda.co.tz: Sasahivi upo nje ya Yanga, ni kitu gani ambacho una-miss kutoka Yanga?

Telela: Kuwa karibu na marafiki ambao tulikuwa tunaishi pamoja siku zote, kuwa nao mbali ni kitu ambacho naki-miss, mbali na hapo maisha yapo kawaida tu.

shaffihdauda.co.tz: Siku moja Yanga wakihitaji huduma yako uwanjani, utakuwa tayari kurejea?

Telela: Wakifata kile nachotaka mimi niko tayari kurudi, popote pale tutakapokubaliana mimi ntacheza sio Yanga pekeake.

Jumatano September 7, Ndanda ilicheza dhidi ya Yanga kwenye uwanja wa Nangwanda, Mtwara na mchezo huo kumalizika kwa suluhu. Telela alicheza kwa mara ya kwanza dhidi timu yake ya zamani (Yanga) akiwa amevalia uzi wa Ndanda, shaffihdauda.co.tz ikaamua kumcheki Telala na ili azungumzie alivyojisikia wakati akipamana na wachezaji wenzake waliokuwa wakicheza pamoja siku za nyuma.

“Kikubwa nachoshukuru tumepata matokeo haijalishi tumecheza na nani, nashukuru tumeonesha ushirikiano kulikuwa hakuna tofauti yoyote uwanjani,” alisema Telela aliyeitumikia Yanga kwa misimu sita mfululizo na kuisaidia kutwaa mataji pamoja na kushiriki michuano ya kimataifa.

Kwasasa Telela anasoma Diploma in Accauntacy kwenye chuo cha St. Augustine University of Tanzania (SAUT) tawi la Mtwara huku akiendelea kukipiga Ndanda FC.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here