Home Ligi EPL GUARDIOLA VS MOURINHO, TUMEWAACHA MUIVUNJE SAHANI.

GUARDIOLA VS MOURINHO, TUMEWAACHA MUIVUNJE SAHANI.

785
0
SHARE

Jose-Mourinho-Pep-Guardiola-672846

Dunia katika soka inaweza kuwa imetekwa na majiji mawili maarufu yaani Real Madrid na Barcelona. Hawa wanafanya wanachotaka na wanashinda wanavyojisikia huku pia wakiwa wamebeba wachezaji wawili bora zaidi katika uso wa dunia hii kupitia Messi na Ronaldo.

Unaweza pia kuamua kusema wachezaji 6 bora zaidi kwa kutizama mtiririko wa tuzo kubwa duniani unavyosema ingawa hilo la kwanza ni sahihi zaidi. Pamoja na yote hayo huwezi kutaja soka bila kuweka neon makocha ambao mbinu zao ndiohuamua ubora wa kila klabu.

Katika hili kuna vichwa viwili ambavyo vimetawala dunia kwa nafasi yao ya kipekee na wanaongelewa kwa utofauti. Mmoja ni yule asiyependa nywele ziishi kichwani kwake huku akiwa sio mzungumzaji anaitwa Guardiola, na mwingine ni yule mwenye nywele nyingi zenye mvi na maneno mengi yenye kuudhi na kejeli anayeitwa Mourinho.

Makocha bora wa kipee na wenye falsafa tofauti ambao hawaishi kuitwa maadui bahati nzuri hata sahani kwa sasa wameigawa katika vipande viwili vinavyolingana na kila mmoja anakula chakula chake yaani wote wapo Manchester moja wakisubiri kuona nani atatawala kuliko mwingine.

Dunia ya habari imekuwa ikitaja zaidi uadui wao kuliko urafiki wao. Wachache wanaokumbuka kuwa watu hawa waliwahi hata kukumbatiana na faraja lakini wengi wanaweza kukumbuka matukio ya kipekee ya kibabe wakati waliofanya mechi ya EL Clasico iwe mechi bora na maarufu zaidi duniani. Wachache wanaweza kuwa na kumbukumbu kuwa hawa walilelewa pamoja chini ya kocha maarufu sana Sir Bobby Robson.

Mourinho alikuwa mkalimani huku Pep akifanya kazi chafu ndani ya uwanja. Kipindi amacho inasemekana moja ya ushindi wa kipekee waliopata Barcelona dhidi ya PSG katika kombe la washindi wa Ulaya, walikumbatiana kwa furaha sana na kupata picha ambayo Mourinho anayo mpaka leo na aliwahi kukiri hilo.

Man Utd boss Jose Mourinho and Man City boss Pep Guardiola

Lakini kuanzia hapo ni kama dunia haikuwahitaji wawe pamoja na ni kama jambo ambalo lilikuwepo hili litokee na maandiko yatimie kwa upande wao kuwa “tizama na watakuwa wapinzani walete burudani ya kipekee kwa mashabiki nje ya Cristiano na Messi”. Mourinho alizaliwa ili amwonyeshe Guardiola na Guardiola alikua hili amwondoe Mourinho, na vita yao iwe ya kipekee.

Si ajabu uhasimu ukawa ulizaliwa ndani ya Barcelona yenyewe kwani ilishasemwa kabla kuwa Mourinho aliishi kuja kuifundisha Barcelona siku moja. Alikuzwa na Robson ilia je kuwa mwalimu ndani ya Barcelona. Na si ajau kuwa moja ya nukuu maarufu za miaka ya 2000 za Mourinho zilisema “moyo wangu upo Barcelona na utaishi hapa kuanzia sasa n ahata milele”.

Baada ya Rijkaard kupewa taarifa ya kuwa mwisho wake ulikuwa umefika, mtu wa kwanza kupata taarufa za nafasi ya ajira alikuwa Mourinho. Ndio, mtu wa kwanza kabla ya Pep, na mtu aliyeonekana anastahili nafasi yoyote kuliko kocha mwingine yoyote.

Wakurugenzi wa wakati huo wa Barcelona, Txiki Begiristain ambaye kwa sasa yupo na Man City pamoja na Marc Ingla walimfanyia usaili Mourinho akiwa Lisbon. Mourinho inasemekana aliwaambia kuwa akipewa nafasi hiyo mtu wa kumsaidia angekuwa Guardiola ambaye alikuwa na kikosi cha timu ya vijana.

Lakini kama kuonyesha walikuwa wana upendo ndani yao, Guardiola ambaye hakuonekana kujua hata kama angepata nafasi ile aliwahi kupendekeza jina la Mourinho kwenye bodi ya uendeshaji ya timu hiyo.Lakini alikuwa na Johan Cruyff aliyekuwa sahihi zaidi na ambaye alikuwa na maono makubwa kuliko wote kwani alibadili upepo wote uliokuwa kusini na sasa vyombo vilipeperushwa kuelekea Kaskazini.

Aliwakumbusha  Begiristain na Ingla kuwa mtu pekee ambaye alikuwa anafanana na Barcelona na Barcelona ilikuwa pacha wake ni Guardiola. Na maamuzi yalibadilika pale na dunia aliyokuwa Mourinho ikasimama kwa muda kwenye mlingoti wake kwani haturajia nap engine hapo ndipo kiapo chake kilipofika ukomo.

Kitu ambacho mkurugenzi Ingla aliwahi kusema ilikuwa sumu ndani ya moyo mgumu wa Mourinho. Sumu ambayo ilionekana pale ambapo Inter Milan ilipoweza kuifunga Barcelona huku Mourinho akishangilia kwa aina ya kipekee kabisa. Dhihaka za kuzungumza mgongoni kwa Pep na kukimbia akizunguka uwanja wa Camp Nou baada ya kuwatoa Barcelona. Ndio kilikuwa kipindi ambacho aliongoza kisasi cha Samuel Eto’o pia dhidi ya mkatalunya huyo.

Madrid iliyokuwa mchovu ikaona mwokozi anaishi nchini Italia katika jiji la Milan na ambaye alimfahamu Guardiola vyema, wakamleta Malaika wa watu wachache katika jina la Mourinho.kipindi ambacho Guardiola aliwaonyesha kuwa mfumo wa vijana ungezishinda fedha nyingi.

Bahati mbaya sana ni kuwa maisha hayakuwa kama yalivytarajiwa kwa upande wa Mourinho kwani moja ya usiku ambao njozi zake hazikuwa sawa ni ule ambao goi tano alizishuhudia zikipita kwenye mgongo wa Iker Casillas na asijue la kufanya. Baada ya hapo ilikuwa historia ambayo jina El Clasico lilianzia kwa mashabiki, wachezaji mpaka makocha.

Kipindi ambacho Madrid alipata kadi nyekundu katika michezo minne mfululizo, huku Mourinho akilaumu mchezo wa kivivu na uongo mwingi wa wachezaji wa Barcelona. Miaka imesogea sana, na inaonekana Guardiola hakuwahi kuridhika huku Mourinho akiwa kama ambaye hakuwahi kuamini. Kila mmoja kamtamani mwenzie, na sasa wote wanatizamana wikiendi hii.

Moja ya michezo ambayo itatoa mwanga wa mwanaume ambaye atakuwa hatua kadhaa kusogelea taji la ligi kuu ya Uingereza. Bahati nyingine ambayo inaweza kutua machoni kwa wapenzi wa soka ni yule mjivuni Zlatan Ibrahimovic. Huyo hakuwahi kukubaliana na Pep Guardiola na hakuwahi kushindana na Jose Mourinho. Anakutana na mbaya wake akiwa kwenye mikono ya kipenzi chake na sasa rafiki wa adui amekuwa adui.

Tunasubiri Manchester Derby, tunasubiri vita ya Mourinho na Pep Guardiola. Hawa tabia zao huwa ni kumeza hata ukubwa wa mechi yenyewe na sasa tunaweza kuwa tumepata mechi kubwa baada ya El Clasico kwa sababu yao. Bahati nzuri wanaufurahia upinzani na hawaonekani kuukataa. Ahsante kwa kuivunja sahani, tunasubiri kuona atakayewalisha wengi, wote nyie si wapishi wazuri?

MOURINHO AKIKUMBATIANA NA GUARDIOLA WAKATI AKIWA KOCHA MSAIDIZI WA BARCELONA

 

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here