Home Kimataifa KIPA DONNARUMMA WA AC MILAN AVUNJA REKODI YA BUFFON.

KIPA DONNARUMMA WA AC MILAN AVUNJA REKODI YA BUFFON.

788
0
SHARE

doon

Kinda wa klabu ya AC Milan, Gianluigi Donnarumma ameweka rekodi ya aina yake na kuvunja ile rekodi iliyokuwa inashikiliwa na kipa Gianluigi Buffon katika timu ya Taifa ya Italia.

Katika mchezo uliofanyika Bari, kati ya timu ya Taifa ya Ufaransa dhidi ya Italy, Donnarumma aliingia kuchukua nafasi ya Buffon katika mchezo ambao Italia walipoteza kwa mabao 3-1.

Donnarumma anakuwa mchezaji mdogo zaidi kuwahi kuichezea timu ya Taifa ya Italia akiwa na umri wa miaka 17 baada ya Buffon kucheza mchezo wake wa kwanza na timu hiyo ya Taifa akiwa na umri wa miaka 19.

Donnarumma alizaliwa siku 484 baada ya Buffon kucheza mchezo wake wa kwanza na timu ya Taifa, Oktoba 29 mwaka 1997. Kinda huyo aliingia kipindi cha pili ambapo Italia walikuwa nyuma kwa mabao 2-1 tayari.

“Buffon aliniambia niingie uwanjani, niwe mtulivu na nifanye yote ninayojisikia kufanya kwa uhuru, yaani niwe huru tu na nifurahie mchezo”, alisema kinda huyo ambaye pia alivunja rekodi ya kuwa kipa mdogo kuwahi kuichezea klabu ya Ac Milan. Donnarumma aliichezea Ac Milan akiwa na umri wa miaka 16 na miezi 8.

Buffon ameweka wazi kuwa anamwona kinda huyu kama mchezaji sahihi anayekuja kuvaa viatu vyake katika lango la timu ya Taifa na anavutiwa sana na kipaji chake. Donnarumma ni mrefu sana katika umri wake kwani tayari ana urefu wa futi 6’5.

Buffo ndiye mchezaji aliyecheza michezo mingi zaidi na timu ya Taifa ya Italia. Amecheza michezo 162 huku pia akiwa mshindi wa kombe la dunia mwaka 2006 yaliyofayika pale Ujerumani.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here