Home Kimataifa PICHA- SCHWEISTEIGER ALIPOSHINDWA KUZUIA MACHOZI YAKE WAKATI AKIAGWA RASMI UJERUMANI JANA

PICHA- SCHWEISTEIGER ALIPOSHINDWA KUZUIA MACHOZI YAKE WAKATI AKIAGWA RASMI UJERUMANI JANA

625
0
SHARE
1Jana Ujerumani walicheza mchezo maalum kwa kirafiki kwaajili ya kumuaga aliyekuwa nahodha wao Bastian Schweinsteiger.
Katika mchezo huo ambao Ujerumani walishinda mabao 2-0 dhidi ya Finland, Schweinsteiger alijikuta akilia kabla ya mchezo huo kufuatia kushindwa kuzuia hisia zake na kutokwa na machozi mbele ya washabiki lukuki waliokuwa wametamalaki uwanjani wakimuaga kwa heshima kubwa lakini wakiwa na huzuni kubwa.
Bastian Schweinsteiger alikabidhiwa kitu mithili ya cheti cha heshima kilichoandikwa ‘Team Player. Leader. Idol.’
Akiwa amekumbatiana na kocha wake wa timu ya taifa Joachim Low kuonesha furaha aliyokuwa nayo
Akitoa hotuba ya kuwaaga mashabiki na wapenzi wa waliofika uwanjani
Akiwa na Rais wa Chama cha Soka nchini Ujerumani Reinhard Grindel
‘Sikutarajia kama ningekuwa na hisia kali kiasi kile,’ Schweinsteiger aliongea wakati akitoa hotuba yake ya kuwaaga. ‘Asanteni nyote kwa ujio wenu. Najisikia ni mwenye furaha na naamini tutazidi kuonana tena siku zijazo.’

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here