Home Kimataifa NGASA ALICHO-POST INSTAGRAM BAADA YA KUVUNJA MKATABA SOUTH AFRICA

NGASA ALICHO-POST INSTAGRAM BAADA YA KUVUNJA MKATABA SOUTH AFRICA

868
0
SHARE

IMG_201609246_010503

Taarifa za Mrisho Ngasa kuvunja mkataba na klabu yake ya Free State Stars FC ya Afrika Kusini zinazidi kuenea kwa kasi hususan kwenye mitandao ya kijamii.

Kwa mujibu wa barua ya kuvunjwa mkataba huo iliyotolewa na Meneja Mkuu Rantsi Mokena inaonesha mkataba huo umevunjwa tangu August 25, 2016 na kwa maana hiyo Ngasa yupo huru kujiunga na timu yeyote watakayofikia makubaliano.

Baada ya taarifa hizo huzidi kusambaa, Ngasa maarufun kwa jina la ‘anko’ ame-post picha inayoonesha akiwa katika timu mbalimbali ambayo imeambatana na ujumbe.

“Thanks God am so happy now, dua zangu umekuwa ukiniitika kila ninapokuita. Picha ipi imekukumbusha mbali hapo ankali,” ni baadhi ya maneno yanayosomeka kwenye post ya Ngasa.

“#I love my Tanzania#am free agent,” hivyo ndivyo Ngasa alivyomaliza.

IMG-20160901-WA0026

Ngasa alisajiliwa na Kina Phiri ambaye alikuwa kocha wa Free State Stars kwa wakati huo, lakini kwa sasa ni kocha wa Mbeya City majukumu aliyopewa baada ya kutimuliwa kwenye klabu hiyo ya nchini Afrika Kusuni.

Wakati anasajiliwa Free State alikuwa ni mchezaji huru akitokea Yanga baada ya makataba wake kumalizika mwishoni mwa msimu wa 2014-15.

IMG-20160901-WA0025

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here