Home Kimataifa MASWALI NA MAJIBU KUHISIANA NA USAJILI KUTOKA INSTAGRAM, YAKIJIBIWA NA NICASIUS

MASWALI NA MAJIBU KUHISIANA NA USAJILI KUTOKA INSTAGRAM, YAKIJIBIWA NA NICASIUS

748
0
SHARE
q&a

q&a

SWALI KUTOKA KWA RICHARD GODRICK

QN= Mpaka sasa timu ipi imefanya usajili mzuri?

JIBU: Richard vilabu vingi vimefanya usajili bora sana lakini binafasi nimevutiwa kwa kiasi kikubwa na usajili wa Antonio Conte. Amesajili eneo ambalo kwa Waitaliano ni eneo linaloheshimika zaidi, yaani eneo la ulinzi. Kumrudisha David Luiz na kumpata beki wa kushoto Alonso kunamaanisha klabu ya Chelsea inaweza kuwa na ukuta mgumu sana katika ligi kuu ya Uingereza. Hii

ikiungana na uwepo wa viungo wakabaji Ngolo Kante na Nemanja Matic. Kumbuka, kuna usemi unasema Attack gives you wins but defense earns you championships, ikiwa na maana eneo la ushambuliaji linakupa ushindi lakini eneo la ulinzi linakuhakikishia ubingwa. Chelsea wanafuatiwa na Man City ambayo haijafanya usajili wa kushitua lakini wachezaji wote waliokuja wataingia kwenye falsafa lakini pia Jose Mourinho kafanya usajili mkubwa wenye tija. Tottenham inaweza kuwa timu yenye usajili wenye tija zaidi kwa kuhahakikisha hawaanguki mbali.

SWALI KUTOKA KWA VALENCE FREDRICK

QN: Hivi kuna tatizo gani kati ya Cesc Fabregas, maana fununu ni kuwa hawaelewani?

JIBU: Mwanzo ilisemekana hivyo, na kikubwa kilikuwa ni kutokupata nafasi kwa Fabregas huku akionekana ni mchezaji ambaye aliwasaidia sana kutwaa ubingwa kwa pasi za mwisho. Baadae Fabregas alikanusha taarifa hizi kwa kusema hana tatizo na Conte na hajaambiwa kuondoka klabuni.

Kiufundi ni kuwa Fabregas hawezi kupata nafasi kwa Conte kwa sababu kubwa moja. Conte ni muumini wa wachezaji wanaojua kukaba vyema hasa eneo la kiungo. Na kwa sababu inawezekana hasiweze kuja na mfumo wa 352 imeonekana kuwa namna pekee ni kutumia viungo wawili wa ukabaji ili kufidia ahitaji ya ukabaji ambayo hupatikana katika 352.

Lakini pia Oscar na Willian ni wazuri kuanzia kukaba eneo la adui kwa maana ya kupress na kwa pamoja wanaweza kukupa kitu anachokupa Fabregas kwa kiasi ila Fabregas hawezi kukupa nguvu kazi ya hawa wawili. Hii ndio sababu Conte hamchezeshi Fabregas lakini haina maana sio mchezaji mzuri. Mahitaji ya mwalimu tu.

SWALI KUTOKA KWA PROSPER PS.

QN: Kuna tofauti kwenye ufungwaji wa dirisha la Usajili kati ya EPL na Bundesliga?

Kwa Ulaya kuna tofauti ndogo sana kwa maana ya ligi kubwa zile. Kwa mfano dirisha la Bundesliga hutangulia kufungwa kwa masaa machache, kisha dirisha la Uingereza halafu dirisha la Hispania na Italia hufuata baada ya Takribani saa moja.

Lakini imekuwepo tofauti ya madirisha duniani kote. Hii inatokana na sababu zilizowekwa na FIFA ambazo hutokana na ushindani wa ligi husika kulingana na michezo mingine kwa mfano ligi ya Marekani hupisha usajili wa michezo mingine kama Mpira wa kikapu na Baseball. Lakini kitu kingine ni hali ya hewa ya eneo husika. Brazil, China nao wamekuwa na tofauti ya dirisha la usajili na nchi za Ulaya. China dirisha la usajili lilifungwa Julai 15.

GIDEON GIBBONCE anauliza kama Arsenal Wachezaji ni Walewale au kuna nyongeza?

Ndugu yangu Gideon unaweza kufurahi sasa kwa maana Arsenal wameongeza beki ambaye kimsingi ni mzoefu na ataongeza kitu kikubwa Shokdrani Mustaffi. Lakini pia Wenger inaonekana anataka kubadili aina ya ushambuliaji na tutegemee kitu kinachoitwa free flowing football kwa maana ya kuachana na Giroud na kutumia wachezaji waliokuwa huru kucheza nafasi nyingi ndani ya uwanja katika eneo la ushambuliaji kwa sababu ya ujio wa Lucas Perez.

JADEF DE VAN VANX anauliza kama Liverpool wamefanya usajili zaidi.

Inaonekana Klopp alifunga usajili na Wjinaldum na hakuna nyongeza tena. Lakini wameondoka jumla ya wachezaji 13 katika kikosi cha Liverpool katika dirisha hili la usajili. Na katika siku ya mwisho wameondoka Luis Alberto kwenda Lazio, Balotelli katua Nice ya Ufaransa na pia Markovic kaenda Sporting Club Lisbon ya Ureno.

THEDONE KIJIKO anauliza kuhusiana na Bastian Shweinstiger kama anabaki na United?

Bastian kaamua kubaki na inasemekana jambo hili limemkera sana kocha Jose Mourinho ambaye alitaka mchezaji huyu ampishe pale kwa maana ya kutokumhitaji. Lakini pia Bastian jana aliagwa katika timu ya Taifa walipocheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Finland hivyo kuwa mchezo wake wa mwisho. Usisahau pia alisema klabu yake ya mwisho kuichezea akiwa Ulaya itakuwa Manchester United kwa maana ndio klabu pekee aliyotaka kuichezea baada ya Bayern Munich.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here