Home Kimataifa Barcelona wafafanua kwanini waliachana na usajili wa Pogba

Barcelona wafafanua kwanini waliachana na usajili wa Pogba

1964
0
SHARE

Barcelona walikuwa na saini ya Paul Pogba mikononi mwao wakati wa kipindi cha kiangazi kilichopita, mchezaji ambaye sasa ameishia mikononi mwa Manchester United katika uhamisho uliovunja rekodi ya usajili duniani. 

Mkurugenzi wa klabu hiyo Albert Soler, ambaye alikuwa Turin wakati Barca wanafanya mipango ya kumsaini Pogba alieleza leo Alhamisi kwamba Barca walifanya mazungumzo na Juventus.
“Mwaka uliopita tulikubaliana na Juve kwamba ikitokea wanataka kumuuza Pogba wakati wa dirisha la usajili kwamba tungepewa kipaumbele – hivyo tulikuwa na nafasi hiyo,” alikiri.

“Braida wa Juventus alitusaidia kutuhakikishia kipaumbele, lakini Juve hawakutaka kutuuzia na sisi hatukjaribu kung’ang’aniza.

“Tulikuwa kwenye kipindi cha uchaguzo na usajili wa aina ya mchezaji kama Pogba isingewezekana kushughulikia na uongozi wa mpito.”

Barça waliamua kutoendelea na biashara ya Pogba kwenye dirisha hili la usajili, kwa sababu tayari walikuwa na usajili wa Denis Suarez na Andre Gomes.

Kwa fedha ambayo United wametumi kumsaini Pogba, na ukiongozea kiasi kingine kidogo – jumla ya fedha imeweza kusaini wachezaji 6 wa Barcelona waliosajili kwenye dirisha hili la usajili.

“Ikiwa tungemsaini Pogba, basi tungetumia €100m kwa mchezaji mmoja.

“Na kwa kiasi cha 122 million euros tulifanikiwa kusaini wachezaji 6. Tumebadili filosofia yetu kiasi: tumesajili wachezaji wenye umri mdogo.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here