Home Kimataifa JOE HART KILA KITU TAYARI TORINO, BADO KUTANGAZWA TU

JOE HART KILA KITU TAYARI TORINO, BADO KUTANGAZWA TU

800
0
SHARE

1Klabu ya Torino inayoshiriki Ligi Kuu nchini Italy ‘Serie A’ muda wowote kuanzia sasa inaweza kutangaza kumsajili kwa mkopo kipa namba moja wa England Joe Hart kutoka klabu ya Manchester City.

Jana mlinda lango huyo alipewa kibali cha kuodoka kambini na Chama cha Soka nchini England (FA) kwenda Torino kufanya vipimo vya afya.

Hart alianza kupata wakati mgumu punde tu baada ya kuwasaili Pep Guardiola na kuambiwa kwamba yuko huru kuondoka endapo itatokea klabu yoyote inayomhitaji.

Hart (29) alionekana kwenye picha jana akiwa jijini Turin na anatarajiwa kukamilisha uhamisho wake kabla ya dirisha la usajili kufungwa leo usiku.

Hart atarejea kujiunga na wenzake kambini kuelekea mchezo wa kufuzu fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018 dhidi ya Slovakia punde tu baada ya usajili wake kukamilika.

Tangu msimu mpya wa EPL uanze, Hart hajacheza hata mchezo mmoja chini ya utawala mpya wa Guardiola ambaye tayari ameshamsajili kipa mpya kutoka Barcelona Claudio Bravo mwenye umri wa miaka 33.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here