Home Kimataifa JE WAJUA? NICASIUS ANAKUJUZA YAFUATAYO

JE WAJUA? NICASIUS ANAKUJUZA YAFUATAYO

980
0
SHARE
Je wajua

nicas

  1. Katika historia ya EPL ni wachezaji wawili tu waliowahi kufunga penati kwa miguu yote. Wachezaji hao ni Obafemi Martins na Bobby Zamora.

ob

2. Assist au pasi pekee ya bao aliyowahi kupiga Super Mario Ballotelli kwenye EPL ilikuwa ya goli la Sergio Aguero dhidi ya Queen Park Rangers lililoipa ubingwa Manchester City.

balo

3. Wayne Rooeny, Gareth Bale na Kevin Davies ndio wachezaji pekee kwenye historia ya ligi kuu ya Uingereza kufunga, kutoa pasi ya bao na kujifunga pia katika mchezo mmoja.

ro

4. Carl Lewis ambaye ni moja ya wanamichezo watatu (mwingine ni Michael Phelps) kuwahi kushinda medali nne za dhahabu kwenye shindano moja la Olimpiki aliwahi kuchaguliwa kujiunga na klabu ya Chicago Bulls mwaka ambao pia Jordan alichaguliwa na klabu hiyo kutoka chuoni. Ilikuwa mwaka 1984. Kama hukulijua hili basi lifahamu.

carl

5. Mwaka 1974, mtendaji mkuu wa klabu ya Atlanta Hawks, Pat Williams alitangaza kuwa katika raundi ya 10 ya kuchagua wachezaji, klabu yake ilimchagua James Williams. Alipoulizwa mchezaji huyu ni nani na anatoka wapi, Williams akajibu, “anatoka hospitali ya Piedmont kule Atlanta; ana urefu wa inchi 19.5, na uzito wa paundi 7.5.” Williams alikuwa amemchagua mwanae ambaye alikuwa kazaliwa siku hiyo. Baada ya ukimya wa sekunde kadhaa, Si Gourdine, ambaye alikuwa msaidizi wa kamishna alisema,  “haikubaliwi.”

pat

Mpaka wakati mwingine. Follow Instagram @nicasiusagwanda

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here