Home Kitaifa KAMUSOKO ADHIHIRISHA MAPENZI KWA MAMA YAKE KWA KUMWANDIKIA UJUMBE ‘MURUA’

KAMUSOKO ADHIHIRISHA MAPENZI KWA MAMA YAKE KWA KUMWANDIKIA UJUMBE ‘MURUA’

890
0
SHARE

IMG_0348

Thabani Scara Kamusoko, kiungo mkabaji na wakati mwingine mchezeshaji ni moja ya wachezaji mahiri na wenye nidhamu kubwa katika klabu ya Yanga.

Uwepo wake kwa kushirikiana na wachezaji wengine ulichangia kuipa Yanga ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Azam Sports Federation Cup pamoja na kufanikiwa kutinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, licha kushindwa kufuzu kwenda nusu fainali baada ya kumaliza nafasi ya mwisho kwenye kundi lao.

Leo mama yake ametimiza umri wake wa miaka kadhaa tangu kuzaliwa, Kamusoko ameamua kumwandikia ujumbe mzuri wa kumtakia heri ya siku hii maalum kwake.

Kamusoko, ambaye pia amekuwa na juhudi kubwa za kujua lugha ya Kiswahili ukilinganisha na wachezaji wengine wa kigeni amemwandikia mama yake ujumbe huo kwa kuchanganya lugha ya Kiswahili na Kiingereza.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Kamusoko ameandika: “Happy birthday mama yangu…..mungu akuongezee maisha marefu…i wish i was there to celebrate with you….love you mama and i mis you.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here