Home Kimataifa Jicho la 3: SIWEZI KUMLAUMU DEO DIDA, UONGOZI HAUKUWA MAKINI CAF 2016…

Jicho la 3: SIWEZI KUMLAUMU DEO DIDA, UONGOZI HAUKUWA MAKINI CAF 2016…

1718
0
SHARE

DSC_0645

Na Baraka Mbolembole

SIWEZI kumlaumu Deogratius Munishi ‘Dida’ kwa kuvaa jezi iliyotengenezwa na kampuni nyingine tofauti na zile walizotumia wachezaji wengine katika game ya Caf Confederation Cup kati ya TP Mazembe ya DR Congo na timu yake ya Yanga SC siku ya Jumanne iliyopita. Lakini kitendo hicho ni wazi kimeonesha sehemu nyingine ya udhaifu, umakini na utayari wa viongozi wa klabu hiyo katika anga za kimataifa.

Nakumbuka wakati Yanga ilipolazimika kuingia dukani kusaka jezi za kutumia saa chache kabla ya kuanza kwa game yao ya kwanza katika hatua ya makundi ya michuano dhidi ya MO Bejaia huko nchini Algeria mwezi June, 2016 niliandika kwamba ni sababu mojawapo iliyowaangusha katika mchezo waliopoteza 1-0.

Jezi ya Deogratius Munishi 'Dida' ikionekana wazi kutengenezwa na kampuni ya Macron (jina hilo linaonekana kifuani kwake upande wa kulia) jezi hiyo ilikuwa tofauti na za wachezaji wengine wao walivaa jezi zilizotengenezwa na kampuni ya Nike
Jezi ya Deogratius Munishi ‘Dida’ ikionekana wazi kutengenezwa na kampuni ya Macron (jina hilo linaonekana kifuani kwake upande wa kulia) jezi hiyo ilikuwa tofauti na za wachezaji wengine wao walivaa jezi zilizotengenezwa na kampuni ya Nike

Licha ya kwamba nilipingwa na mashabiki wa klabu hiyo, ukweli ni kwamba uongozi wa timu haukuwa umejiandaa kwa matukio muhimu ya nje ya uwanja. Wakati ule (June) Yanga walishindwa kupeleka kiongozi yeyote katika semina elekezi ya Caf-Shirikisho la soka Afrika.

Timu zote 8 zilizokuwa zimefuzu kwa robo fainali zilitakiwa kuhudhuria semina hiyo elekezi lakini Yanga pekee walipuuza ndiyo maana hawakuwa wakifahamu taratibu za michuano hiyo. Juzi ni mshangao zaidi kwa maana uongozi wa timu uliruhusu Dida avae jezi zilizotengenezwa na kampuni ya Macron tofauti na Nike ambazo ziliwavaliwa na wachezaji wa nafasi nyingine!

Benchi la ufundi nalo lilivaa jezi zilizotengenezwa na kampuni ya Macron (sawa na Dida) tofauti na zile zilizovaliwa na wachezaji wengine
Benchi la ufundi nalo lilivaa jezi zilizotengenezwa na kampuni ya Macron (sawa na Dida) tofauti na zile zilizovaliwa na wachezaji wengine

Ndiyo, haijulikani kama Yanga wana mkataba na Nike au la, ila kitendo cha Dida kuvaa jezi za kampuni nyingine ni dhahiri kabisa kimedhihirisha kuwa uongozi haukuwa makini katika kipindi chote cha michuano hiyo ambayo walishinda game moja na kuambulia sare moja katika mechi zao 6.

Kwa namna timu ilivyokuwa ikicheza ndani ya uwanja, benchi la ufundi na wachezaji walikuwa makini kwa muda wote wa michuano lakini kwa uongozi ni tofauti.

Matukio mengi, kununua jezi za dharura Algeria, mizozo ya utawala wa klabu na TFF, kisha hili la Dida ni mambo ambayo Yanga wanapaswa kuyachukulia kama funzo unapokuwa katika hatua ya juu ya michuano ya kimataifa.

Picha ya kikosi cha Yanga inayoonesha tofauti ya jezi ya Dida na jezi za wachezaji wengine wa kikosi hichohicho
Picha ya kikosi cha Yanga inayoonesha tofauti ya jezi ya Dida na jezi za wachezaji wengine wa kikosi hichohicho

Licha ya kujiita ‘Wakimataifa’ Yanga wameshindwa kudhihirisha hilo kwa vitendo hasa katika utawala. Inawezekana ni jambo la kawaida tu kwa watu wengine, lakini siamini kama David De Gea anaweza kuingia uwanjani akiwa amevaa jezi iliyotengenezwa na kampuni tofauti na ile atakayovaa Zlatan Ibrahimovic pale Manchester United.

Ndani ya uwanja, naamini Yanga ni kati ya timu 16 bora za michuano yote ya Caf 2016 (Champions league na Confederation Cup) na wamedhihirisha kwa vitendo kwa kuwa miongoni mwa timu 8 bora za Confederation Cup 2016, ila katika uongozi mambo mengi yameendeshwa katika kiwango cha michuano ya Cecafa Kagame Cup.

Siwezi kumlaumu Deo Dida kwa kuvaa jezi iliyotengenezwa na kampuni tofauti na zile walizovaa wachezaji wenzake, lakini watu wa ng’ambo wanaweza kushangazwa na hilo.

Kwa ukaribu zaidi, tafadhali unaweza ku-LIKE PAGE yangu #BSports Tanzania . Utapata Updates za michuano mbalimbali

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here