Home Ligi EPL ACHA NIMPELEKA MAMADOU SAKHO KWA WENGER

ACHA NIMPELEKA MAMADOU SAKHO KWA WENGER

1106
0
SHARE

Mamadou Sakho

Na Athumani Adam

Chanzo kimoja cha kimataifa kimeripoti kwamba shirikisho la kupambana na madawa michezoni (Wada) hawatokata rufaa kupinga uamuzi wa shirikisho la mpira wa miguu barani Ulaya (Uefa) kuhusu ile ya kesi ya kutumia madawa yaliopigwa marufuku michezoni  iliyokuwa ikimkabili beki wa Liverpool mfaransa Mamadou Sakho.

Wakati Sakho akifurahia taarifa hiyo kuna tetesi za Meneja wa Liverpool, Jurgen Klopp kutaka kumtoa Sakho kwa mkopo kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili barani Ulaya jambo ambalo limewafanya baadhi ya  mashabiki wa Liverpool kutokubaliana na uamuza wa kocha wako.

Kimatazamo sio kwamba Sakho ameshuka kiwango kulinganisha na mabeki waliopo Liverpool. Huyu Dejan Lovern ambaye anaanza kwa sasa kwenye kikosi cha kwanza cha Liverpool hakuwa chaguo la kwanza la kocha Jurgen Klopp. Hata kipindi cha Brendan Rodgers kuanzia September msimu wa 2015/16 Sakho alikuwa chaguo la kwanza mbele ya Lovern.

Ukichunguza vizuri utagundua kwamba Klopp bado ana mipango na Sakho, kwanza alimpa jezi mpya wakati wa maandalizi ya msimu lakini anamtoa kwa mkopo badala ya kumuuza moja kwa moja.

Nadhani kinacholendea sasa ni mwendelezo wa ule mgogoro kati ya Jurgen Klopp na Mamadou Sakho wakati wa maandalizi ya msimu mpya wa Ligi kule nchini Marekani ndio sababu ya kutolewa kwa mkopo. Klopp aliwahi kukaririwa akisema Sakho anakiuka taratibu zilizowekwa na  timu kuhusu chakula, mazoezi pia aliwahi kuchelewa ndege.

Yawezekana Sakho kuwa na matatizo kweli sababu hii sio mara ya kwanza kuingia kwenye mgogoro dhidi ya kocha wake. Aliwahi kukorofishana na Brenden Rodgers alipoachwa kwenye kikosi ambacho kilipambana dhidi ya Everton miaka miwili iliyopita japo baadae  aliomba radhi na kurudi kikosini.

Wakati Klopp akimuondoa Sakho ambaye aikuwa tegemeo kwa takribani misimu mitatu tangu atue Anfield kutoka PSG naona  ni fursa pia bahati  kwa kocha wa Arsenal, Arsene Wenger kumchukua Sakho kwa mkopo  kuziba nafasi zilizopo kwenye safu ya ulinzi ya Arsenal kutokana na mabeki wake tegemeo kuwa majeruhi.

Bila shaka Wenger anahitaji beki mwingine mzoefu, nadhani Sakho ni chaguo sahihi miongoni mwa machaguo mengi ambayo Wenger anayo kwa sasa hususan kipindi hiki ambacho dili la kusajili Shkodran Mustafi kutoka Valencia linaeleka kufeli kama lilivyofeli dili la Jimy Vardy kutoka Leicester.

Nafikiri Sakho  ni bora zaidi  ya John Evans ambaye Wenger anahusishwa na tetesi za kupeleka ofa ya kutaka kumsajili kwa thamani ya Euro milioni 25.

Msimu uliopita Sakho alikuwa muhimili kwenye safu ya ulinzi ya Liverpool, alikaba kwa ufasaha, alianzisha mashambulizi kutoakana na pasi zake za uhakika kwenye mechi zote 21 alizocheza kwenye ligi kuu ya England. Akasaidia Liverpool kufika hatua ya fainali michuano ya Europa ligi

Kama Klopp anataka kumtoa Sakho kwa Mkopo alafu Wenger anaamini kinda  Robert Holding ndio chaguo la kuziba  nafasi ya Per Metersaker, au  Char Chambers ni ndio mbadala wa Laurent Koscienly basi acha nimpeleke Mamadou Sakho kwa mkopo kwa Wenger kabla ya kufungwa dirisha la usajili barani ulaya.  sidhani kama nitakuwa nimekosea sana.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here