Home Kimataifa MESSI KURUDI ARGENTINA NI SOMO KWA VIONGOZI NA MASHABIKI

MESSI KURUDI ARGENTINA NI SOMO KWA VIONGOZI NA MASHABIKI

517
0
SHARE

Messi-Argentina

Na Mahmoud Rajab

Lionel Messi amerudi, ndiyo amerudi, hajafika mbali alipotaka kwenda akaamua kurudi. Messi ameamua kurudi tena kulichezea taifa lake pendwa la Argentina baada ya kutangaza kustaafu punde tu baada ya kupoteza kwa penati mchezo wa fainali ya Copa America Centenario dhidi ya Chile.

Licha ya kufikia hatua ya kufanya maamuzi hayo, Messi bado hajakosa hata mchezo mmoja iwe ni kimaishindano au wa kirafiki. Kurejea kwake kwenye timu hiyo ya taifa maarufu kwa jina la Albiceleste kumepokewa kwa bashasha kubwa na wapenzi wa soka nchini humo. Lakini hili sasa linatakiwa kuchukuliwa kwa namna ya kipekee sana safari hii.

“Ni wakati mgumu sana kuuelezea,” alisema Mess wakati Copa America ilipomalizika. “Kitu cha kwanza ambacho kunanijia akilini mwangu ni kwamba imetosha. Kwangu mimi, suala la timu ya taifa sasa nimemaliza. Nimecheza fainali nne sasa. Ndicho kitu nilikuwa nakipigania, lakini kimeshindikana. Nadhani ndiyo hivyo. Ninachojisikia sasa ni huzuni kubwa. Nimekosa penati, aah ndiyo hivyo tena.”

Messi pia akaongeza: “Nafanya hivi kwa nia njema kwa kila mtu. Kwangu na kwa wengine wote. Wengi wanapenda hivyo.”

Hata hivyo, ameona kwamba wakati wengi wakitaka aondoke, lakini wengi zaidi walitaka arudi na yeye kuamua kufikiria upya uamuzi wake.

Wakati mwingine huwezi kutambua thamani ya kitu mpaka kiwe hakipo, sasa hili ndilo lililotokea kwa Messi, wengi walionekana kuwa na huzuni kubwa baada ya kutoonekana kwenye mapokezi ya kikosi cha taifa hilo. Mwanzoni alikuwa akilaumiwa kukosa kuipa timu ubingwa badala ya kupongezwa kwa kitendo chake cha kuifikisha timu fainali, na hiyo haikuwa fair kwake hata kidogo.

Messi alikutana na kocha mpya wa Argentina Edgardo Bauza jijini Barcelona Alhamisi ya wiki hii, na hata kama kocha huyo aliwaambia waandishi kwamba hawakujadili juu ya kurejea kwa staa huyo kwenye timu ya taifa, lakini punde tu baada ya kuonana naye ndipo Messi alipotangaza kurejea na sasa atajumuika kwenye kikosi cha Argentina kwenye michezo ya kufuzu kucheza Kombe la Dunia dhidi ya Uruguay na Venezuela mwezi Septemba.

Na siku ya Ijumaa sasa ndiyo taarifa rasmi ya uthibitisho ilitoka.

“Naona kuna matatizo mengi kweye soka la Argentina na nisingependa kuongeza mengine zaidi,: Messi alisema kwenye taarifa yake ya kurejea kuchezea timu ya taifa.

“Nisingependa kusababisha hatari yoyote, siku zote nimekuwa nikijaribu kufanya vitu tofauti kuisaidia timu yangu vyovyote niwezavyo. Tunapaswa kuondoa matatizo mengi kwenye soka la Argentina, na ningependa kufanya hivyo nikiwa ndani ya timu kuliko nje ya timu.”

“Wakati wa fainali ile, nilikuwa na msongo wa mambo mengi sana kichwani mwangu na kikukweli niliamua kuachana na timu ya taifa, lakini mapenzi yangu kwa nchi hii na hii jezi yamenifanya nirudi, nadhani punde tu tutaanaza kufurahia matunda kwa pamoja,”

Na sasa Messsi amerudi, anahitaji mapenzi mazito na sapoti kubwa sana kutoka kwa Wa-argentina wenyewe ili awafanyie kile wanachohitaji.

Kocha wa zamani wa Chile ambaye kwa sasa anafundisha Sevilla, mwaka jana alinukuliwa akisema: “Ninachoweza kusema ni kwamba Leo Messi akiwa Argentina hachezi kama ambavyo hucheza akiwa Barcelona kwasabau pengine hana furaha kama anayoipata Barcelona.

Hilo ni tatizo kubwa ambalo kocha wa sasa wa Argentina Bauza atakuwa akikabiliana nalo, huku Chama cha Soka nchini Argentina (AFA), watahitajika pia kuhakikisha wanayashughulikia yote ambayo Messi alikuwa akiyalalamikia hasa kwenye Michuano ya Copa America ya mwaka huu iliyofanyika nchini Marekani.

Ndani na nje ya uwanja, Argentina wanapaswa kumfanya Messi awe na furaha zaidi hata aliyokuwa nayo awali. Huku wakikabliwa na harakati za kufuzu kucheza Kombe la Dunia mwaka 2018, hii ni fursa ya mwisho kwa mchezaji huyo ambaye pengine ni bora kuwahi kutokea kwenye historia ya soka ulimwenguni kwa muongo mmoja sasa. Messi amejitahidi kwa kadri ya uwezo wake kulifanyia mema taifa lake. Sasa ni muda wa washabiki, maofisa wa AFA, wachezaji wenzake na kila mmoja anayeguswa na taifa hilo moja kwa moja kuhakikisha wanafanya kila juhudi ili Messi awape wanachokihitaji.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here