Home Ligi EPL UFUNGUZI WA LIGI YA UINGEREZA KWA UNDANI WAKE

UFUNGUZI WA LIGI YA UINGEREZA KWA UNDANI WAKE

723
0
SHARE

epl

Kuanzia leo tarehe 13 Aug mpaka 28 Aug, Pep Guardiola na Man City yake watakuwa na michezo 5, pamoja na ile ya Ulaya.  Karibu katika Epl Pep, huu ndio mfano wa yanayotokea mwezi Desemba, mtunze sana Aguero. Nimeketi nawaza Leroy Sane, Silva na Kevin De Bryune nyuma ya Aguero. Kuna kila dalili kiatu kikawa halali ya Aguero, kwanini usifunge?

Leicester City wamemleta Nampalys Mendy kuwa mbadala wa Kante. Ranieri anamkubali sana huyu, tatizo kazi aliyoifanya Kante msimu uliopita, alikuwa Messi wa eneo lake. Ukifananishwa nae ni mzigo. Wapinzani mtizameni sana Musa, nahisi kasi yake itawanyanyasa wengi hasa wale watakaokuwa wanamtizama Mahrez na Vardy pekee. Huyu atawaongezea Leicester City hatari zaidi wakati wa kushambulia kwa kushitukiza (counterattacks).

Umewatizama Middlesbrough? Ujinga uliwafanya wasipande msimu uliopita lakini huu wamo.  Ndio timu ya kuchungwa zaidi kwa upande wangu kwa hizi zilizopanda daraja msimu huu. Wana tabia za mkia wa mbuzi, ni wasumbufu tu na muda wote hawatulii.

Tottenham wamemleta Vincent Jansen. Mguu wa dhahabu kutoka ligi ya Eredivisie kule Uholanzi. Maombi yao yote wayaweke katika huyu kuelewana na Harry Kane. Akifanikiwa basi wapinzani wana kesi ya kujibu. Sitamani kuyaona ya Soldado.

Everton wanahitaji Muda kiasi lakini nahisi Koeman atafanya mabadiliko makubwa sana kwenye Ulinzi, walikuwa wabovu sana msimu uliopita. Nakupa siri tu, tegemea kuzaliwa upya kwa Kevin Mirallas msimu huu.

Kuna mambo mawili kwa Southampton. Aidha wakafanya vibaya sana au wakawashitua wengi. Napenda muonekano wa kikosi chao, kikubwa unawapa nafasi ya kufanya biashara kubwa msimu ujao. Naamini watafanya vyema ingawa nafasi waliyofika msimu uliopita ni ngumu kuifikia. Wameacha wazoefu kadhaa muhimu sana.

Moja ya vitu vya kushangaza katika ligi kuu ya Uingereza ni kubadilika ghafla kiuchezaji kwa klabu ya Stoke City. Wametoka kuwa mabuldoza mpaka walaini. Kwa sasa ni walaini na wananyumbulika kuliko hata Liverpool na Manchester United. Hawa silaha yao kubwa sio wachezaji wao, silaha yao kubwa ni akili ya Mark Hughes.

Ni ngumu sana kufanya vyema kwa kubadili falsafa haraka vile lakini kaweza. Msimu wa pili wa Shaqiri na Anaurtovic pamoja na uwepo wa Imbula na Allen katikati mwa uwanja. Usitegemee kwenda kupata point kirahisi pale BET 365, hili ni jina jipya la uwanja wa zamani Britannia Stadium. Kunanuka damu.

Hull City wanaishi kama Ndanda ya Tanzania, tofauti ndogo sana. Hawana usajili wa maana waliofanya na wanaanza ligi bila kocha mkuu. Wasiporudi walikotoka ni mafanikio makubwa.

Tukutane kesho kwa uchambuzi wa michezo hiyo. Ligi inaanza kesho. Usisahau kuffolow Instagram @nicasiusagwanda

Nicasius Nicholaus Agwanda (Coutinho Suso)

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here