Home Kimataifa GENK YABANWA MBAVU LIGI YA UBELGIJI

GENK YABANWA MBAVU LIGI YA UBELGIJI

587
0
SHARE

KRC Genk

Klabu ya KRC Genk anayoitumikia Mtanzania Mbwana Samatta, Jumamosi August 13 imeshindwa kutamba mbele ya Waasland Beveren baada ya kubanwa na kulazimishwa sare ya kufungana magoli 2-2 kwenye mchezo wa ligi ya Ubelgiji.

Genk walitoka nyuma kwa magoli 2-0 hadi kusawazisha magoli yote na kuambulia pointi moja katika mchezo huo. Nikolaos Karelis aliifungia Genk goli la kwanza dakika ya  35 kabla ya mchezaji wa Waasland Beveren Laurent Jans  kujifunga na hatimaye kuisawazishia Genk. Magoli ya Waasland Beveren yalikwamishwa kambani na Ibrahima Seck aliyefunga dakika ya 6 na Jonathan Buatu ambaye alifunga bao la pili.

Katika mchezo huo Samatta aliingia dakika ya 47 kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Kebano.

Mechi hiyo ilikuwa ni ya tatu katika ligi ya Ubelgiji (Belgian Jupilier Pro League) ambapo hadi sasa Genk inakamata nafasi ya 6 ikiwa na pointi tatu baada ya kucheza mechi tatu ikifanikiwa kushinda mechi moja, sare moja huku ikipoteza mchezo mmoja.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here