Home Kitaifa DIDA ATAJA SABABU ZINAZOIDHOOFISHA YANGA KIMATAIFA

DIDA ATAJA SABABU ZINAZOIDHOOFISHA YANGA KIMATAIFA

903
0
SHARE

IMG_201608226_080142

Mchezo wa nane bora kati ya Yanga dhidi ya MO Bejaia unatarajia kupigwa jioni ya bleo kwenye uwanja wa taifa, wakati Yanga inaingia uwanjani kutupa karata yake ya tano ikiwa na pointi moja, ikumbukwe Yanga ilifungwa bao 1-0 kwenye mchezo wa awali uliopigwa Algeria.

Mlinda mlango wa Yanga Deogratius Minishi ‘Dida’ ameuzungumzia mchezo dhidi ya MO Bejaia: “Tuanawaomba mashabiki wetu wasikate tamaa, tupo pamoja nao hii ndiyo timu yao na wanatakiwa kuja kuipa sapoti mwanzo mpaka mwisho. Wanatakiwa wajivunie timu yao kufika katika hatua hii, ni jambo la heshima waendelee kuiamini timu yao na kuiunga mkono Mungu akitujaalia kwenye mechi dhidi ya MO Bejaia tunaweza kupata ushindi.”

Inaonekana kwama mmetawaliwa na uchovu kwasababu hamjazoea kucheza kwa muda mrefu,imekuwa kawaida ligi ikimalizika mnapumzika .

“Hilo kweli lipo lakini tutajitahidi tuweze kupata hata ushindi kwenye mechi moja lakini naamini madaktari wetu na waalimu wanazidi kutupa nafasi ya kupumzika na kutupa huduma za hapa na pale ili tuwe vizuri siku hadi siku. Mimi naamini tangu tumeingia kwenye mashondano haya, tumekutana na changamoto kadhaa kama kusafiri mara kwa mara, mazoezi mfululizo na mechi mfululizo, lakini ni fundisho kwetu kwenye msimu ujao.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here