Home Ligi EPL ARSENE WENGER: NAOGOPA KUSTAAFU

ARSENE WENGER: NAOGOPA KUSTAAFU

518
0
SHARE

Mzee

Arsene Wenger amesema kwamba mustakabli wake ndani ya Arsenal unategemea na matokeo ya timu hiyo baada ya msimu huu wa ligi kukamlizika, lakini akasisitiza kwamba ataendelea kubaki kwenye soka bila kujali nini kitatokea

Wenger amebakisha mwaka mmoja tu kwenye mkataba wake na Arsenal huku akiwa ameshaitumikia klabu hiyo kwa miaka 21 sasa

Mfaransa huyo, ambaye amesema kwamba hatafanya maamuzi yoyote kuhusu mustakabali wake mpaka msimu ujao, alisema: “Nitakachoifanyia timu ndicho kitategemea mustakabali wangu.”

“Huwezi kujua. Unapaswa kufanya kazi kama ndio maisha yako ya kila siku, lakini pia unapaswa kujua muda wowote ule unaweza kuacha,” amesema.

Wenger amesema kwamba anaogopa sana kustaafu.

“Nitakachokifanya ni kuendelea kufanya kazi ili mradi tu bado nina nguvu  za kufanya kazi, bila kujali ni kazi gani. Siku zote nitafanya kazi tu.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here