Home Ligi EPL MAN UNITED HII, KUNA ZLATAN HALAFU KUNA MOURINHO

MAN UNITED HII, KUNA ZLATAN HALAFU KUNA MOURINHO

643
0
SHARE

Mou-Zlatan

Na Mahmoud Rajab

Jose Mourinho ni moja ya makocha ambao wamejaa ari ya ushindi, ni kocha anayejua afanyeje ili apate ushindi, ni kocha ambaye anajua apite wapi ili achukue taji au ubingwa wowote kwa njia yoyote.

Amefanya hivyo akiwa Chelsea katika kipindi chake cha mwanzo, amefanya hivyo alivyorudi kwa mara ya pili kabla ya mambo kumwendea kombo na kutimuliwa.

Tujikumbushe kidogo wakati akirudi Chelsea kwa mara ya pili. Msimu wa kwanza wakati anafika alisema kwamba, nia yake ilikuwa ni kujenga timu kwaajili ya msimu uliofuata na hakika alifanya hivyo. Unajua msimu wa pili alifanya nini? alimleta Costa, Fabregas na Drogba akiwa tayari sasa kuchukua taji la EPL.

Wengi walishangaa ni kwanini alimrejesha Drogba. Mourinho anajua aina ya wachezaji ambao wamejaa ari ya ushindi na moyo wa ushindani. Sasa Drogba licha kwamba umri ulikuwa umemtupa mkono, lakini Mourinho alijua nini sababu hasa ya kumleta na bila shaka mchango wake ulionekana kwa namna aliwatia hamasa vijana na ufanikiwa kuchukua taji la EPL baada ya kulikosa kwa muda mrefu.

Bahati mbaya msimu uliiopita hakufanya vizuri na ndipo Abramovic alipomfungisha vilago.

Aliamua kukaa benchi kwa muda kabla ya kuelekea msimu mpya wa ligi kutangazwa kuwa kocha wa Man United. Kama alaivyofanya akiwa Chelsea, Mourinho amefanya usajili wake wa kisayansi baada ya kuleta damu changa kama beki wa kati Eric Bailly, amemleta Henrikh Mkhtaryan, Pogba yuko njiani sasa na kubwa zaidi ni pale alipoamua kumleta Zlatan Ibrahimovic.

Uamuzi wake uliwatia wasiwasi wengi wakisema kwamba mshambuliaji huyo Msweden umri wake umemtupa mkono, na kutokana na ugumu wa ligi ya England itamuwia vigumu.

Wakati anamsajili Mourinho alisema: Nimemleta Zlatan

kwasababu ni mshindi, mimi ni mshindi na sote tunajua tunataka ushindi. Popote tuendako huwa tunashinda. Na hapa tutashinda.”

Hiyo ndiyo kaluli ya kiburi kabisa aliyoitoa Mourinho juu ya ujio wa Zlatan. Unajua kwenye mchezo wake kwanza kabisa kuvaa jezi ya United alifanyaje? unajua vizuri, ilikuwa dhidi ya Galatasaray na alifunga goli lake la kwanza la na ufunguzi katika mchezo tena kwa staili ya bicycle kick.

Hapo alianza kuwaonesha nini Man United wamekosa kwa muda mrefu. Mourinho alianza kuwaziba mahasimu wake midomo.

Sasa jana kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Leicester, wakati matokeo yakisomeka 1-1 na huku zikiwa zimesalia dakika saba tu kabla ya mchezo kumalizika, Msweden huyo kwa mara nyingine tena akaonesha kwanini alisema atakuwa Mungu wa United. Akapachika goli la pili kwa kichwa mujarab baada ya kupata krosi maridhawa kutoka kwa mchezaji anayerudi kwenye ubora wake Antonio Valencia na kumwacha kipa Kasper Schmeichel akiwa hana la kufanya.

Huyu ndiyo Ibra halisi, Ibra anayejua nini akifanye na wakati gani mbele ya lango. Ni kweli hakuwa na mchezo mzuri sana kutokana na kutokuwa na muunganiko mzuri hasa kwenye sehemu ya ‘final third’, lakini yeye ndiyo alikuwa na maamuzi ya mwisho katika mchezo huo. Na hivyo sasa ndivyo Mourinho na Zalatan mwenyewe wanavyopoenda kufanya hasa ukiangalia kwenye maeneo mengi waliyopita.

Baada ya mchezo ule, wachezaji wenzake waliounda kundi dogo na kuanza kumpongeza na kumshukuru sana kwa kile alichokifanya. Wanajua fika kwamba wamepata bahati kubwa kuwa na nguli huyo wa soka, huku wakitumaini kuona mabadiliko makubwa kwenye timu yao msimu huu.

United walikuwa wakiongoza hapo awali. Goli lao la ufunguzi lilifungwa na kijana yule yule aliyewapa ushindi katika mchezo wa FA wakati huo wakiwa chini ya Louis van Gaal, lakini safari hii kulikuwa na ladha tofauti kabisa.

Jesse Lingard alionesha ule umuhimu wa mchezaji kuwa na hadhi ya kuichezea United. Aliwavuruga mabeki wanne wa Leicester kabla ya kumchambua kipa Schmeichel na kuwapa United goli la uongozi. Kupewa kwake nafasi ya kuanza dhidi ya Henrikh Mkhitaryan lilikuwa ni jambo la kushangaza kidogo, lakini goli lake lilionesha nini Mourinho anakusudia kufanya msimu huu na kuwapa ndoo ya EPL Man United.

Kwa ujumla, japokuwa United hawakucheza kwa kiwanho kikubwa sana. Lakini walionesha kwamba chini ya Mourinho kuna kitu kizuri kinakuja msimu huu.

Baada ya mchezo huo, Mourinho alisema kwamba matokeo yale ni ya kifame na Zlatan ndiyo mhusika mkuu wa ushindi huo wa Ngao ya Jamii, huku akigusia pia suala la ujio wa Pogba, ambapo taarifa zilizoenea jana zilidai kwamba alikuwa akifanyiwa vipimo vya afya kwa ajili ya kujiunga na klabu hiyo.

Tutegemee kuona makubwa sana msimu huu na hakika, kwa United hii chini ya Mourinho, halitakuwa jambo la kushangaza.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here