Home Kimataifa KIPRE TCHETCHE AAHIDI KURUDI AZAM

KIPRE TCHETCHE AAHIDI KURUDI AZAM

738
0
SHARE

Azam vs Ruvu JKT

Mshambuliaji wa kimataifa wa Ivory Coast Kipre Tchetche ameandika ujumbe wa kuwaaga mashabiki wake wa klabu ya Azam FC mara baada ya kukamilisha dili lake la kuhamia klabu ya Al Nadha ya nchini Oman.

Kupitia account yake ya instagram Tchetche aliandika ujumbe kuwashuru mashabiki, pamoja na uongozi mzima wa Azam FC  kwa kumsapoti katika kipindi chote cha miaka mitano aliyohudumu katika klabu hiyo inayozidi kukuwa kisoka.

Tafsiri isiyo rasmi ya ujumbe huo inasomeka hivi: “Miaka mitano Dar es Salaam, Tanzania, nchi iliyonipa furaha wakati nikicheza soka, viongozi waliniunga mkono kwenye nyakati zote nzuri na mbaya,” sehemu ya ujumbe wa Tchetche inasomeka hivyo.

“Sitawasahau mashabiki walionipenda na kutinia moyo hata wakati sipo katika kiwango kizuri, asante Azam FC kwa yote hapa ni nyumbani, siku moja nitarudi.”

“Sitaaacha kusema Azam imenifanya nipige hatua kwenye soka lakini, ulifika muda wa mimi kuondoka. Nitaukumbuka uwanja wa Chamazi, uwanja ambao nilikuwa nikifunga magoli na kushinda mechi, asanteni sana.”

“Azam ipo moyoni mwangu milele.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here