Home Kimataifa DRAYMOND GREEN AYAZUA, NIDHAMU YAKE YAZUA MASWALI.

DRAYMOND GREEN AYAZUA, NIDHAMU YAKE YAZUA MASWALI.

636
0
SHARE

green

Draymond Green ameibuka katika siku za karibuni kama mmoja wa wachezaji walioleta mapinduzi kwenye mchezo wa mpira wa kikapu kwa nafasi anayocheza huku akionyesha kuwa mhimili mkubwa wa klabu yake ya Golden State Warriors.

Green ameleta ladha ya kuonyesha muda mwingine kutokuhitaji watu warefu kucheza katika eneo la Centre ambalo limezoeleka kuwepo kwa big man yaani mchezaji mwenye kimo kirefu. Lakini pamoja na umuhimu huu bado Greena amekuwa mchezaji ambaye tabia zake haziridhishi.

Ndani ya uwanja na kwenye vyumba vya kubadilishia nguo inaamimika kuwa Green na kiongozi kutokana na hisia zake na uwezo wa kuongoza wengine kwa mfano katika ushindani dhidi ya timu pinzani lakini hii bado haikuzuia kukumbana na utata kadhaa kutoka kwake.

Mwanzo Green alionekana kumpiga teke kwenye sehemu za siri mchezaji Steven Adams wa klabu ya Oklahoma City Thunders wakati wa fainali za kanda ya Magharibi. Hakuishia hapo alionekana pia kurusha mkono kumpiga Lberon James sehemu za siri jambo ambalo lilipelekea kufungiwa mchezo mmoja na ambayo inaaminika kuwa sababu ya Warriors kupoteza hasa baada ya kukosekana pia kwa Andrew Bogut.

Mapema tu baada ya fainali kumalizika Green alikamatwa kwa kosa la kumpiga na kumdharilisha mtu, lakini alifanikiwa kuepuka kifungo. Lakini mapema wiki hii huku akiwa katika kambi ya timu ya Taifa ya Marekani kujifua na mashindano ya Olympic, Green kalizua tena.

Draymond Green ameweka picha ya sehemu zake za siri katika mtandao wa kijamii wa Snapchat, picha iliyokaa kwa takribani dakika kumi kabla haijaondolewa. Green baadae aliomba radhi akisema sehemu kama mitandao ya kijamii ukikosea kubonyeza mara moja tu unajikuta umetuma vitu sehemu isiyokuwa sahihi. Akaenda mbali zaidi na kudai kuwa picha ile ilikuwa siri na ilikuwa inatumwa kwa siri na sio kwa watu wote kuona.

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here