Home Kitaifa KUFUNGWA NOMA SANA, CHIFU WA KAUZU KALOWA ‘CHAPACHAPA…’

KUFUNGWA NOMA SANA, CHIFU WA KAUZU KALOWA ‘CHAPACHAPA…’

759
0
SHARE

IMG_0182

Chifu wa Kauzu ni shabiki wa Ndondo ambaye amejizolea umaarufu mkubwa kutokana na style zake za ushangiliaji huku akipata mashabiki wengi wanaopenda vituko na mbwembwe zake pindi anapokuwa anaishangilia timu yake Kauzu FC.

Watu wengi walikuwa wanasubiri kuona Chifu ataingiaje kwenye mechi ya fainali kati ya Kauzu dhidi ya Temeke Market, na imekuwa ni utamaduni wake kuingia uwanjani tayari mechi ikiwa imeanza au mechi inapokuwa mapumziko.

Chifu aliingia uwanjani akiwa amekaa kwenye chungu hii ikiwa ni mwendelezo wa kuwania tuzo ya kikundi bora cha ushangiliaji lakini pia ikiwa ni burudani kwa mashabiki wa Ndondo Cup.

Leo ameingia uwanjani dakika chache kabla ya mapumziko, ile kuingia tu uwanjanini timu yake (Kauzu) ikapigwa bao la tatu lakini bado hakuonesha kuwa na wasiwasi. Akawatuliza mashabiki wa Kauzu kwa kuowaoneshea ishara ya vidole vitatu kwamba goli zitarudi, dakika chache baadae Kauzu ikapata goli lakini mwisho wa siku mchezo ukamalizika kwa matokeo hayo ya Kauzu kufungwa bao 3-1.

Chifu agaeuka kocha

Wakati dakika zikiendelea kuyoyoma huku Kauzu ikiwa nyuma kwa magoli 3-1 dhidi ya wapinzani wao Temeke Market, Chifu hakutaka tena habari za kushangilia badala yake akabadilisha majukumu na kuwa kocha . Alianza kutoa maelekezo na kuhamasisha wachezaji kitu ambacho kilimfanya awe kivutio kwa mashabiki bila yeye kujua.

IMG_0179

Tambo zamtokea puani

Siku chache kabla ya mchezo wa fainali, timu ya Sports Extra ilipiga kambi mitaa ya Tandika kwenye maskani ya Kauzu FC na kuzungumza na viongozi pamoja na mashabiki wa timu hiyo. Kwa upande wa Chifu yeye aliahidi kombe lazima litue Kauzu lakini mwisho wa siku haikuwa hivyo, baada ya dakika 90 kumalizika kombe likaenda Temeke Market na kumwacha Chifu akiduwaa kwa mara ya pili mfululizo baada ya msimu uliopita kupigwa pia na Faru Jeuri kwenye game ya fainali.

IMG_0157

Chifu apotea ghafla

Kawaida ya Chifu ni kuzungumza na vyombo vya habari mara baada ya mechi kumalizika, lakini baada ya mchezo wa fainali Chifu alitoweka na waandishi wasijue amepotelea wapi. Waandishi wengi walitaka kujua Chifu yuko katika hali gani baada ya kupoteza fainali ya pili mfululizo na angesema nini laki jitihada za kumpata ziligonga mwamba.

Eti hainaga ushemeji…

Market na Kauzu ni timu za Temeka na zinatenganishwa na mitaa kadhaa, kwahiyo wanaukaribu na wanafahamiana vizuri ndani na nje ya uwanja. Baada ya leo Temeke Market kuwala Kauzu kwa ugali wa dona, wimbo wa Man Fongo ndiyo aliokuwa akiimbiwa Chifu na mashabiki wa Market kila walipomuona Chifu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here