Home Kimataifa OFFICIAL: HIGUAIN NI MALI YA JUVENTUS

OFFICIAL: HIGUAIN NI MALI YA JUVENTUS

695
0
SHARE

Higuaini

Juventus wamekamilisha dili lao la kumsajili Gonzalo Higuain kutoka Napoli kwa ada ya euro mil 90.

Higuain alikuwa akihusishwa kwa muda mrefu kujiunga na miamba hiyo ya Italy baada ya kukamilisha mazungimzo binafsi mwanzoni mwa mwezi July.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina (28), amesaini mkataba wa miaka mitano kwa mabingwa hao wa Serie A walio chini ya Massimiliano Allegri, ambapo atakuwa akivuta kitita cha euro mil 7 kwa mwaka.

Higuain, ambaye msimu uliopita alifunga mabao 36 kwenye michezo 35, alijiunga na Napoli mwaka 2013 na kusaini mkataba uliokuwa ukimalizika June 2018. Sasa ataunga na mastaa wengine kama Miralem Pjanic, Marko Pjaca, Medhi Benatia na Dani Alves ambao wote wamejiunga na Kibibi kizee hicho cha Turin kwenye majira haya ya usajili wa kiangazi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here