Home Kitaifa YANGA YAPAA KUIFATA MEDEAMA

YANGA YAPAA KUIFATA MEDEAMA

1023
0
SHARE
Kocha wa Yanga Hans Pluijm akiiingia ndani ya uwanja wa ndege
Kocha wa Yanga Hans Pluijm akiiingia ndani ya uwanja wa ndege
Kocha wa Yanga Hans Pluijm akiiingia ndani ya uwanja wa ndege

Kikosi cha Yanga kimeondoka kuelekea nchini Ghana kwa ajili ya mchezo wake wa marudiano wa kombe la shirikisho Afrika dhidi ya Medeama.

Yanga watashuka uwanjani Julai 26 siku ya Jumanne kucheza mechi yao ya pili ugenini baada ya kucheza mechi mbili pia nyumbani.

Matheo Anthony akiwa na Ally Mustapha 'Barthez' Uwanja wa Ndege
Matheo Anthony akiwa na Ally Mustapha ‘Barthez’ Uwanja wa Ndege

Mchezo kati ya Medeama dhidi ya Yanga utachezwa kwenye uwanja wa Essipong Sports uliopo kwenye mji wa Sekondi, Ghana. Mechi hiyo itasimamiwa na mwamuzi wa kati Redouane Jiyed atakayesaidiwa na Mohamed Lahmidi (line one) na Hicham Ait Abboou (line two).

Yanga itaingia uwanjani kupambana na Medeama ikiwa na kumbukumbu ya kutoka sare kwenye mchezo wa awali ilitoka sare ya kufungana goli 1-1 na kujiweka kwenye mazingira ya kusonga mbele kwenye hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo.

Mkuu wa Msafara kutoka ndani ya Yanga Hussein Nyika ambaye ni pia ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji (kulia) akizungumza na manahodha wa timu hiyo Nadir Haroub 'Cannavaro' na Haruna Niyonzima
Mkuu wa Msafara kutoka ndani ya Yanga Hussein Nyika ambaye ni pia ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji (kulia) akizungumza na manahodha wa timu hiyo Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Haruna Niyonzima

Klabu hiyo ya mtaa wa Twiga na Jangwani, ipo nafasi ya mwisho kwenye Kundi A ikiwa na pointi moja kundi ambalo linaongozwa na TP Mazembe ya DR Congo yenye pointi saba ikifatiwa na MO Bejaia ya Algeria yenye pointi tano huku Medeama yenyewe ikiwa nafasi ya tatu kwa pointi zake mbili.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here