Home Kitaifa ROMA, CHIEF WA KAUZU, WAPAGAWISHA SPORTS EXTRA LIVE -TANDIKA

ROMA, CHIEF WA KAUZU, WAPAGAWISHA SPORTS EXTRA LIVE -TANDIKA

590
0
SHARE

IMG-20160723-WA0001

Mkali wa Bongo Hip Hop Roma Mkatoliki jana usiku alip[agawisha mashabiki wake wa Tandika wakati kipindi cha Sports Extra kikiruka live kutoka mitaa ya Tandika kwenye makao makuu ya Kauzu FC.

Asikwambie mtu kulikuwa raia wa kutosha ambao walijitokeza kushuhudia kipindi hicho cha michezo kikiruka moja kwa moja kutoka mtaani kwao. Umekuwa ni utaratibu kwa watangazaji wa Clouds FM husan kipindi cha Sports Extra ambao ndiyo waandaji wa michuano ya Ndondo Cup kufanya kipindi chao live kwenye makao makuu ya timu ambazo zimefuzu hatua ya nusu fainali na kuendelea.

IMG-20160723-WA0010

Baada ya kusubiri kwa hamu kubwa, hatimaye Roma alishika ‘kipa’ na kuanza kuchana hit song zake zote tangu kitambo hadi sasa, mashabiki sasa walipagawa nyota huyo kutokana na kum-miss kwasababu ni muda sasa umepita tangu Roma apige show hadharani.

Mpango mzima sasa ilikuwa ni pale Roma alipo kabidhi mic kwa Chief wa Kauzu, watu wakatarajia jamaa labda ni mkali wa style za ushangilia, lakini namna ambavyo Chief alivyotambaa na beat kila mtu alijikuta akipiga kelele. Hakuna aliyetegemea kama Chief ni mkali wa michano pia, kila mtu aliduwaa kutokana na kipaji cha jamaa huyu ambaye umaarufu wake umekuwa mkubwa kutokana na style mbalimbali za ushangiliaji anazokujanazo kwenye michuano ya Ndondo.

IMG-20160723-WA0004

Jana Sports Extra ilikamisha ziara yake ya kufanya vipindi live kwa kuzitembelea timu nne zilizofuzu kucheza nusu fainali ya Ndondo na matangazo hayo ya moja kwa moja yataendea baada ya kuzifahamu zimu zilotinga hatua ya fainali ya mashindano hayo.

IMG-20160723-WA0009

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here