Home Kimataifa MASTAA WATANO WALIOFIA MIKONONI MWA MOURINHO

MASTAA WATANO WALIOFIA MIKONONI MWA MOURINHO

750
0
SHARE

5.Mohamed Salah

Salah 1

Mohamed Salah alijiunga na Chelsea January 2014, kipindi cha pili cha kocha huyo aliyefukuzwa kwa mara nyingine na miamba hiyo ya London Magharibi.

Mourinho alivutiwa na kiwango chake akiwa FC Basel, lakini hakumpa nafasi ya kutosha kucheza kwenye kikosi cha Chelsea. Alijikuta akikaa benchi karibu msimu mzima uliofuata. Mwishiwe akatolewa kwa mkopo kwenda Fiorentina, na baadaye Roma.

4.Juan Cuadrado

Cudrado

Wakati Cuadrado anajiunga na The Blues January 2015 kwa kiasi cha paundi milioni 26 alitarajiwa kutengeneza pacha ya hatari na Eden Hazard.

Hata hivyo alishindwa kung’aa. Alijikuta kwenye wakati mgumu kwenye mechi yake ya kwanza na kushindwa kumvutia Mourinho. Aliwekwa benchi na baadae kutolewa kwa mkopo kwenda Juventus.

Chini ya kocha wa sasa wa Manchester United, Cuadrado alicheza mara 13 pekee kwenye msimu wa 2014/2015 huku akishindwa kufunga goli hata moja.

3.Juan Mata

Mou mata

Kumuweka benchi Juan Mata wakati wakiwa Chelsea lilikuwa ni moja ya kosa kubwa alilofanya Mourinho katika maisha yake ya ukocha.

Mata alishinda tuzo kama mchezaji bora wa klabu hiyo msimu wa 2012/2013, lakini Mourinho alimtupa benchi msimu uliofuata baada ya kutua kwenye klabu hiyo kabla ya kutimuliwa kwa mara ya pili.

Mhispania huyo baadae alijiunga na Manchester United na tangu hapo amefunga magoli mengi (22) akiwa na mashetani wekundu magoli mengi zaidi kuliko alivyokuwa Chelsea ukilinganisha na muda aliokaa United.

Hivi karibuni, Morinho alitangazwa kuwa kocha wa Manchester United, Je, atamuweka benchi kwa mara nyingine? Tusubiri kuona.

2.Iker Casillas

Casiklas

Casillas alikuwa golikipa namba moja wa timu ya taifa ya Hispania na klabu ya Real Madrid tangu mwaka 2000, lakini Mourinho hakujali heshima aliyojiwekea golikipa huyo pale alipoamua kuanza kumkalisha benchi alipokuwa kocha wa Real Madrid.

Baadaye golikipa huyo aliamua kujiunga na FC Porto mwaka uliopita.

1.Nuri Sahin

Nuri Sahin

Sahin alikuwa anatarajiwa kuwa nyota baadaye baada ya kujiunga na Real Madrid akitokea Borussia Dortmund mwaka 2011, Mourinho hakumpa muda wa kutosha na mturuki huyo aliishia kurudi kwenye klabu yake ya zamani.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here