Home Kitaifa PICHA 20: SPORTS ETXRA ILIVYORUKA LIVE KUTOKA MAKAO MAKUU YA TEMEKE MARKET

PICHA 20: SPORTS ETXRA ILIVYORUKA LIVE KUTOKA MAKAO MAKUU YA TEMEKE MARKET

902
0
SHARE

IMG_0110

Asikwambie mtu Ndondo inabamba sana kitaa, kuelekea nusu fainali ya michuano hiyo, Sports Extra ya Clouds FM inaruka moja kwa moja kwenye makao makuu ya timu ambazo zimefuzu kucheza hatua hiyo.

Baada ya jana kufanya kweli kwenye timu ya Makumba, ikafika zamu ya Temeke Market ambapo timu nzima ya Sports Extra ilikuwa pale kwenye soko la Temeke maarufu kama ‘stereo’ kufanya kipindi kutoka pale huku mamia ya wapenzi wa Temeke Market wakijitokeza kuungana na watangazaji katika kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa.

Temeke Market watacheza mechi yao ya nusu fainali ambayo itapigwa Jumamosi Julai 23 kwenye uwanja wa Bandari kutafuta timu ambayo itafuzu kucheza fainali ya Ndondo msimu huu.

Kuelekea katika kipute hicho, Market wametamba kulipa kisasi kwa kuisambaratisha Makumba wakidai bahati waliyopata Makumba msimu uliopita ya kuwafunga dakika za lala salama mwaka huu haitakuwepo, wamejipanga vizuri timu yao ipo kambini wanachosubiri ni muda tu.

“Tumejipanga vizuri, timu yangu ipo kambini Kisiju inakamilisha maandalizi kwa ajili ya mchezo wa Jumamosi dhidi ya Makumba. Makumba wasitarajie kushinda siku hiyo kwasababu msimu uliopita walitufunga kwa bahati kwa goli lao la dakika za majeruhi lakini msimu huu hawatoki lazima wakae,”  alisema kocha wa Temeke Market.

Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Temeke (TEFA) amesema mwaka huu lazima kombe libaki Temeke kwasababu tangu mashindano yameanzishwa zimebadilisha timu za Kinondoni na Ilala lakini wailaya ya Temeke bado haijafanikiwa kutwaa taji hilo na nafasi yao ni mwaka huu.

“Mwaka huu na sisi lazima tubebe kombe hili, naziamini timu zangu ambazo tayari zimeingia nusu fainali na mimi nazipa changamoto kwamba, watu wa Temeke wanataka kombe kwasababu wenzetu wa Ilala na Kinondoni tayari wameshachukua ubingwa huo  tumebaki sisi tu,” amesema mwenyekiti wa TEFA.

Kesho kama kawaida Sports Extra itafanya balaa jingine maeneo ya Tandika makao makuu ya Kauzu FC hukohuko wilaya ya Temeke. Wakazi na wadau wote wa Kauzu jitokezeni kwa wingi lakini kwa walio mbali wanaweza kufatilia matangazo ya moja kwa moja kupitia Clouds FM kuanzia saa 3:00 usiku.

Mashabiki wa wakiwa wamepagawa na muziki wa Man Fongo ambaye alikuwepo Temeke Sokoni kutoa burudani kwa mashabiki waliojitokeza kuungana pamoja na watangazaji wa Clouds FM wakati wanarusha kipindi cha Sports Extra live

Mtangazaji wa Sports Extra Yahaya Mohamed (mwenye T-shirt ya njano) akirunka kisingeli na mashabiki
Mtangazaji wa Sports Extra Yahaya Mohamed (mwenye T-shirt ya njano) akiruka kisingeli na mashabiki
Man Fongo (katikati) akiwapagawisha mashabiki wake kwa masongi ya singeli
Man Fongo (katikati) akiwapagawisha mashabiki wake kwa masongi ya singeli
Mbwembwe za mashabiki wa Temeke Marketi
Mbwembwe za mashabiki wa Temeke Market
Yahaya Mohamed akifanya mahojiano na Mwenyekiti wa chama cha soka wilaya ya Temeke
Yahaya Mohamed akifanya mahojiano na Mwenyekiti wa chama cha soka wilaya ya Temeke
Mashabiki wa Temeke Market wakiwa wametulia wakifatilia matangazo ya moja kwa moja ya kipindi cha Sports Extra
Mashabiki wa Temeke Market wakiwa wametulia wakifatilia matangazo ya moja kwa moja ya kipindi cha Sports Extra

IMG_0098

Mtunzi wa wimbo rasmi wa Ndondo Cup msimu huu Mnywa maziwa akifanya yake
Mtunzi wa wimbo rasmi wa Ndondo Cup msimu huu anayefahamika kwa jina maarufu la Mnywa maziwa akifanya yake
Kocha wa Temeke Market akiwathibitishia mashabiki wa timu yake kwamba timu yao itabeba ndoo ya Ndondo
Kocha wa Temeke Market akiwathibitishia mashabiki wa timu yake kwamba timu yao itabeba ndoo ya Ndondo

IMG_0086 IMG_0112 IMG_0127

Mtu mzima Mbwiga Mbwiguke akifanya balaa lake, palikuwa hapatoshi
Mtu mzima Mbwiga Mbwiguke akifanya balaa lake, palikuwa hapatoshi

IMG_0120 IMG_0142 IMG_0110 IMG_0137 IMG_0104 IMG_0077

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here