Home Kitaifa KAPOMBE AAHIDI MAKUBWA AZAM FC

KAPOMBE AAHIDI MAKUBWA AZAM FC

617
0
SHARE
Mlinzi wa pembeni wa Azam FC Shomari Kapombe akitolewa nje ya uwanja kwa machela baada ya kuumia kwenye moya ya mchezo wa VPL msimu huu
Mlinzi wa pembeni wa Azam FC Shomari Kapombe akitolewa nje ya uwanja kwa machela baada ya kuumia kwenye moya ya mchezo wa VPL msimu huu

Baada ya kuanza mazoezi mepesi, beki kisiki wa Azam FC Shomari Kapombe ameushukuru uongozi wa klabu hiyo kwa kuwa nae karibu katika kipindi chote alichokua nje ya uwanja kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Kapombe alikosa asilimia kubwa ya michezo ya mwishoni mwa msimu uliopita kutokana na matatizo ya mapafu, ambayo yalimsababishia kusafiri hadi Afrika Kusini kwa ajili ya kufanyiwa matibabu.

Kapombe amesema hana budi kuushukuru uongozi wa Azam FC, kwa jambo la kiungwana walilomfanyia la kuwa nae pamoja katika kipindi cha matibabu yake, hivyo amewaahidi viongozi wake atalipa fadhila kwa kupambana uwanjani.

Mbali na uongozi wa Azam FC, pia Kapombe amewashukuru wachezaji wenzake ambao pia walionyesha kumjali na kumfariji kutokanana matatizo yaliyokua yakimkabili.

“Naushukuru uongozi wa Azam FC, wachezaji wenzangu kwa dua zote walizokuwa wananiombea ili niweze kupona na kurudi salama hicho ni kitu kikubwa ambacho nashukuru nimeweza kurudi.”

“Daktari aliniambia baada ya miezi mitatu naweza kuanza mazoezi lakini naweza kuanza taratibu, na matarajio yangu ilikuwa ni kurudi tarehe 18 mwezi 7, mpaka sasa nimemaliza mapumziko yangu vizuri na natarajia kuanza kazi taratibu huku nikiangalia afya yangu inakwendaje.”

“Nawashukuru pia makocha wapya kwa jinsi walivyonipokea tangu nimerudi kutoka kuumwa, wamenipokea vizuri sikutarajia kitu kama hiki lakini kila mtu alikuwa na furaha kuona nimerudi nikiwa vizuri.”

“Nawaahidi kwamba, nitafanya kazi kama msimu uliopita na nitaitetea timu yangu kwa kile ambacho msimu uliopita tulianguka basi msimu huu tukipate.”

Katika hatua nyingine Kapombe ameelezea kwa undani maradhi yaliyomsababishia kukaa nje ya uwanja kwa kipindi cha miezi mitatu kabl ya kurejea tena katika mazoezi mepesi katika viunga vya Azam Complex huko Chamazi jijini Dar es salaam.

“Kwa muda mrefu nimekaa nje tangu mwezi wa 4, 2016 nikisumbuliwa na ugongwa wa damu kuganda kwenye mapafu uliogundulika baada ya kwenda Afrika Kusini kufanyiwa vipimo na baadae kuanza matibabu.”

Kapombe anaendelea kukumbukwa kwa juhudi binafsi alizozionyesha msimu uliopita, na kufanikiwa kuwa beki pekee wa klabu za ligi kuu ya soka Tanzania bara aliyefunga mabao mengi kuliko mwingine yoyote akitupia wavuni mabao manane huku katika mechi zote ilizocheza Azam FC akicheka na nyavu mara 12 na kutoa pasi za mwisho saba.

Kapombe aliyecheza jumla ya dakika 3188 msimu uliopita katika mechi zote ilizocheza Azam FC.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here