Home Kitaifa JULIO ATOBOA SIRI YA ‘MIZENGWE’ NDANI YA MWADUI, VIPI KUHUSU KUTAKIWA NA...

JULIO ATOBOA SIRI YA ‘MIZENGWE’ NDANI YA MWADUI, VIPI KUHUSU KUTAKIWA NA AZAM FC?

741
0
SHARE
Jamhuri Kihwelu 'Julio'-Kocha Mwadui FC
Jamhuri Kihwelu ‘Julio’-Kocha Mwadui FC

Kwa mara ya kwanza kocha mkuu wa Mwadui FC, Jamuhuri Kiwelu Julio amefichua siri ya ‘mizengwe’ aliyowahi kukutana nayo kwenye klabu ya Mwadui FC ambayo alifanikiwa kupandisha daraja msimu wa 2014-15 na kucheza ligi kuu msimu wa 2015-16.

Julio amesema alikutana na mikasa hiyo kutokana na baadhi ya maafisa wa klabu hiyo kuchoshwa na ukweli aliokua akiwaeleza ili kuondokana na siasa za soka la Bongo ambazo amekua akizipiga vita tangu alipokabidhiwa kikosi cha Mwadui FC mwaka 2013.

Julio amesema alipambana na kufanikiwa kuwashinda watu hao wachache kwa kuangalia maslahi ya Mwadui FC ambayo kwa msimu huu wa mwaka 2016-17 amedhamiria ichukue ubingwa wa Tanzania bara kwa mara ya kwanza.

“Kulikuwa  na figisu kubwa sana na mimi nimebaki kwa kubahatisha sana kwasababu ya watu wa juu, nimsifie sana Katibu wangu alikuwa akinisihi maneno yakisemwa wewe tulia ‘usipaniki’, lakini vilevile Mwenyekiti wangu Joseph Karasa ni mtu ambaye anabusara, anajua kuishi na watu, mvumilivu na anjua vitu anavyovifanya.”

“Unawezaje kusema Julio sio kocha wakati niliipandisha timu kucheza ligi kuu nikadhulumiwa, mwaka uliofata nikaipandisha timu daraja na imemaliza katika nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi na nimecheza nusu fainali ya FA Cup nikatolewa na Azam kwa penati.”

“ Kwa sifa hizo unawezaje kusema mimi sifai? Ndiyo maana nakwambia watanzania wanafigisu, mimi napendwa na wakubwa wa juu, sasa watu wanaona hakuna mtu wa ‘kuni-over power’ ndiyo maana kunakuwa na figisu za hapa na pale.”

“Lakini kingine wasaidizi wangu wa karibu wanajisahau, mimi nimesoma kwa level zote. Ninesoma preliminary, nimesoma intermediate, nimesoma license C, B na sasahivi nina A lakini nina diploma nimepata mbili Brazil moja Holand. Kwahiyo kwenye vyeti tu unawezaje kuniambia mimi sio kocha, kumbuka mimi nimecheza Simba kwahiyo nimefundishwa na walimu wengi, kuwa kwangu juu na mcheshi watu wanachukua vibaya na kutengeneza chuki.”

Kutokana na mkasa huo Julio akafikia hatua ya kutoboa siri nyingine iliyokua imejificha katika maisha yake ya ukufunzi wa soka, kwa kusema aliwahi kupigiwa upatu wa kukabidhiwa kikiosi cha Azam FC lakini bado alikutana na mizengwe ya baadhi ya maafisa wa klabu hiyo.

“Mi nimeshatakiwa Azam kama mara tisa, lakini kila nikitakiwa naambiwa huyo anagawa timu lakini ukienda upande mwingine unaambiwa ukitaka kocha ambaye anafanya motivation na kuwajenga wachezaji kisaikolojia nenda kwa Julio.”

“Lakini mtu kwa kuona huyu akienda atatumeza, ndio maana nakuwa sitakiwi.”

“Yusuf ‘mshkaji wangu’ namshukuru sana kapambana kwa nguvu sana mimi niingie katika timu ya Azam lakini watu wamenipiga mizengwe sana, neno la mwisho alilosema ni kwamba, wewe Julio ni ndugu yangu tumetoka mbali, tusaidiane matatizo mengine lakini hii timu achana nayo.”

“Ndiyo maana mimi hadi leo namkubali kwasababu ni mtu mkweli na anasaidia sana vijana.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here