Home Ligi EPL BYE BYE GIGGS, KUNA MENGI YA KUKUMBUKWA NA KUJIFUNZA KATIKA SAFARI YAKO...

BYE BYE GIGGS, KUNA MENGI YA KUKUMBUKWA NA KUJIFUNZA KATIKA SAFARI YAKO MAN UTD

685
0
SHARE

Giggs 1

Na Naseem Kajuna

Jumamosi asubuhi mashabiki wa Man Utd walipokea habari ambayo walikuwa wakiitegemea kwa mda mrefu. Ryan alitangaza kuondoka ndani ya klabu hiyo.

Ni mashabiki wachache sana ambao wana kumbukumbu ya Man Utd bila Ryan Giggs ambaye aliichezea klabu hii kwa mara ya kwanza mwaka 1991.

Matt Busby alikuwa kocha wa Man Utd kwa miaka 24, Alex Ferguson miaka 27 lakini uhusiano wa Giggs na klabu ya Man Utd umedumu kwa kipindi cha miaka 29, kwani Giggs alisajiliwa na klabu hii akiwa na miaka 14 tu.

Safari yake mpaka kufikia hapa haikuwa bila mabonde lakini. Giggs aliweza kufikia vilele vipya, kuvunja rekodi baada ya rekodi , lakini pia kuchukiwa na watu Old Trafford mda mwingine.

Kama vile mashabiki wa England wachaguapo kusahau mara zote zile walipomzomea gwiji wao David Beckham, mashabiki wa Man Utd mara nyingi husahau wakati ule ambapo kiwango cha Giggs kilishuka na alipokuwa anapata majeraha mara kwa mara na hata pale ilipoonekana kama ataikacha klabu hiyo kwenda kucheza mpira Italy.

Tukiangalia siku hizi za karibuni, mashabiki wengine wa United walimgeukia Giggs kwa nafasi aliyochangia kama kocha msaidizi wa Man United. Mpira wa Man Utd chini ya Van Gaal ulikuwa unakera na mashabiki walikuwa wanataka Giggs aongeze jitihada. Jukumu la kuiokoa Man United liliwekwa kwenye mabega yake na alishindwa ndiyo mtazamo wa wengine, na hawaoni tabu kutofautisha Giggs yule kabla ya kustaafu na yule baada ya kustaafu.

Kiukweli haikuwa haki kutegemea Giggs kufanya zaidi ya kile alichokifanya, kwani isingekuwa sawa kwa msaidizi wa kocha kumsema kocha hadharani. Hamna shabiki ajuaye nini kinaendelea nyuma ya pazia, nini kisemwachwo na majukumu gani Giggs alipewa na kocha. Siyo haki kumsema kwa vitu ambavyo yeye hana maamuzi navyo.

Giggs aliamini kuwa yeye ndiye angekuwa mrithi wa Man United kutoka kwa Van Gaal na uamuzi wake wa kuondoka klabu hiyo bada ya kutua kwa Mourinho kama kocha unaeleweka.

Kama Van Gaal angeweza kutimiza yale aliyoyataka kufanya na kufuta kabisa maovu ya Moyes na kuirudisha Man United tena kileleni, labda Giggs angekuwa mrithi mzuri baada ya Van Gaal kuondoka. Lakini mambo hayakuwa hivyo na Man United haikutaka kucheza bahati nasibu na Giggs kama kocha wao licha ya kuwa Ferguson na wengine waliamini kuwa Giggs ana uwezo wa kuwa kocha bora, na wakaamua kuchagua kocha wa uhakika na anayeaminika, japo tusisahau kwamba Mourinho naye alishawahi kuomba na kunyimwa kazi hiyo zamani.

Kuondoka kwa Giggs kunaashiria kwamba hatokuja kuwa kocha wa Man United sasa kwani kama United ilitaka kumpa kazi hiyo ingempa kazi hiyo mapema kabisa kama ilivyokuwa kwa Pep Guardiola Barcelona na Zinedine Zidane Real Madrid

Giggs

Ndoto ya Ryan Giggs ambaye ameshabikia klabu hiyo maisha yake yote, kutoka kuwa mchezaji nyota mpaka kocha nyota wa klabu hiyo imefikia mwisho. Hakika kama kuna mchezaji yeyote ambaye alistahili kufanikisha ndoto hii ni Ryan Giggs.

Lakini mabaya yote ambayo Ryan Giggs amekutana nayo Man United yamezidiwa na mafanikio.

Tukikumbuka historia yake kama kocha na Mchezaji, kuna nyakati zingine ambazo zinakumbukwa zaidi. Goli lake kwenye mechi yake ya kwanza dhidi ya City, alipotoka nusu ya wachezaji wa Arsenal kufunga goli la kumtoa Arsenal kwenye FA Cup katika dakika za nyongeza, alipovunja rekodi ya  Bobby Charlton ya kucheza mechi nyingi zaidi katika uzi wa Man United katika siku hiyohiyo ambayo aliyofunga penati ya mwisho dhidi ya Chelsea na kuipa man United ushindi wa ligi ya mabingwa.

Wengi waliamini kuwa usiku ule jijini Moscow ndiyo ingekuwa mechi yake ya mwisho Man United na hakika ingekuwa njia nzuri sana kuiaga timu hiyo. Alikuwa na miaka 34 kwa wakati ule na alikuwa ametoka kwenye msimu ambao aliamua kubadilika kutoka kucheza winga mpaka katikati tena kwa mafanikio. Ilionekana kama Giggs aliweza kupata mafanikio yote kwenye mpira na hakukuwa na jipya lakini Giggs hakuishia hapo kwani alicheza misimu mingine 6 akashinda ligi nyingine tatu na akafunga magoli mengine 24.

Giggs hakumbukwi kwa makombe tu, anakumbukwa zaidi kwa kile alichokuwa akifanya kila aingiapo uwanjani. Inabidi uangalie mechi zake za zamani ili ugundue kasi ya ajabu aliyokuwa nayo enzi hizo. Kila wiki Giggs alikuwa akifanya mabeki kuonekana wajinga ama ‘kuwabakisha na damu iliyokunjika’ kama alivyoelezea Ferguson.

Kama siyo kasi yake itakayokuzidi basi ni uwezo wake wa kuweka mipira sumu ndani ya box ambayo ilikuwa ikiwapa mabeki wakati mgumu sana kuikoa. Pia Giggs alikuwa na hamu kubwa sana ya kushinda. Zaidi ya hayo yote lakini Giggs alikuwa akiwakilisha vyote vile ambavyo klabu ya Man United inasifika , ule utamaduni uliowekwa na Busby na baadaye Ferguson. United wanapenda wachezaji wadogo wajitume na kuchukua nafasi yao pale inapokuja, kuisaidia klabu kutwaa makombe na wapatapo mafanikio wawe waaminifu kwa klabu hiyo. Giggs alitimiza vyote hivi.

Giggs 2

Hakika hakutokuwa na mchezaji atakeyapata mafanikio kama ya Giggs United wala hata klabu nyingine yeyote England. Hakuna mchezaji ambaye ataweza kushinda Ubingwa wa England mara 13, kushinda ubingwa wa Ulaya mara mbili na FA Cup mara nne. Hakuna mchezaji ambaye atakaa kwenye klabu yake ya utotoni mpaka atapostaafu na baadaye kukaa kama kocha msaidizi wa klabu hiyo  na hata kupewa ukocha wa muda.

Giggs ni mchezaji wa aina yake na mashabiki wa United wa kizazi hiki hakika wanabahati kusema kuwa walikuwepo kuona safari yake, na hakika safari yake ilikuwa nzuri. Bye Bye Giggs.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here