Home Kimataifa BREAKING NEWS: MESSI AHUKUMIWA KWENDA JELA MIEZI 21

BREAKING NEWS: MESSI AHUKUMIWA KWENDA JELA MIEZI 21

615
0
SHARE

Messi-Jela

Mchezaji wa Argentina na Barcelona Lionel Messi amehukumiwa kifungo cha miezi 21 jela kwa makosa ya ukwepaji kodi.

Baba yake pia amehukumiwa kifungo cha kwenda jela kwa makosa hayohayo ya udanganyifu wa Euro milioni 4.1 (paundi ml 3.5; dola ml 4.5) kati ya mwaka 2007 na 2009.

Hata hivyo, hakuna uwezekano wa mmoja kati ya wawili hao kutumikia kifungo chochote.

Kwa mujibu wa mfumo wa kisheria wa nchini Uhispania, kifungo cha chini ya miaka miwili kinachukuliwa kama onyo (unakuwa chini ya uangalizi maalum).

Jana Jumatano mahakama ya jijini Barcelona iliwatia hatiani Messi na baba yake kwa makosa ya ukwepaji kodi kwa miezi mitatu.

Messi amepigwa faini ya euro mil 2 na baba yake euro mil 1.5.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here