Home Kitaifa KATIBU MKUU BMT AIPAMBANISHA NDONDO CUP NA VPL

KATIBU MKUU BMT AIPAMBANISHA NDONDO CUP NA VPL

470
0
SHARE
Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Tanzania Mohamed Kiganja (katikati) akifatilia kwa makini mchezo wa Ndondo Cup hatua ya 16 bora kati ya Misosi FC vs Wauza Matari kwenye uwanja wa Bandari, Tandika
Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Mohamed Kiganja (katikati) akifatilia kwa makini mchezo wa Ndondo Cup hatua ya 16 bora kati ya Misosi FC vs Wauza Matari kwenye uwanja wa Bandari, Tandika

Baada ya jana Waziri mwenye dhamana ya michezo Nape Nnauye kuhudhuria kwenye michuano ya Sports Etra Ndondo Cup, leo Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Mohamed Kiganja amejitokeza pia kwenye uwanja wa Bandari maeneo ya Tandika ambako leo kulipigwa pambano la 16 bora kati ya Misosi FC dhidi ya Wauza Matairi.

Kiganja amesifu mashindano ya Ndondo Cup kutokana na michuano hiyo inavyoendeshwa huku akiyataja baadhi ya mambo muhimu ambayo ameyaona hadi sasa ndani ya Ndondo Cup.

“Kwanza niwapongeze waandaji, nimpongeze Dr. Mwaka na akina Shaffih wamekuwa wakiyazungumzia haya mashindano na kuwafanya watanzania kuelekeza macho na masikio yao kwenye Ndondo Cup,” amesema Kiganja mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa hatua ya 16 bora kati ya Misosi FC dhidi ya Wauza Matairi.

“Lakini kama Ndondo Cup ingechezwa sambamba na ligi kuu, nadhani watu wangekuja zaidi hapa kuliko huko kuna vitu vingi ambavyo nimeviona kwenye mashindano haya,” Kiganja alisema baada ya kuvutiwa na viwango vya wachezaji wa Ndondo Cup.

“Hakuna mchezaji kutoka nje, wote wanacheza hapa ni wachezaji wa kitanzania, sidhani kama kuna mchezaji anayetoka nje. Hilo ni la kwanza, unakuja kuangalia mpira halisi wa kitanzania. Kwahiyo mchezaji bora, mfungaji bora wote ni watanzania.”

“Maandalizi ya mashindano ni mazuri, watu wanapata kile wanachostahili. Hakuna kuzungurushana, mchezaji bora wa kila mechi anapata zawadi yake, kama kuna kuna timu bora inapata zawadi, timu iliyoshinda na iliyofungwa zote zinapata zawadi na zawadi ziko wazi. “

“Hii ndiyo sehemu pekee kwa vijana wetu wanapoweza kuonekana, lakini pia vijana wetu watumie fursa hii kwa ajili ya kujiuza kwenda kucheza mbele zaidi, wasifikirie hapa ndiyo mwisho bali waende mbele zaidi. Kwasababu waliowaandalia walikuwa na lengo baada ya mashindano vijana hawa wawe sehemu fulani.”

Katika mchezo huo, Misosi FC wamefanikiwa kufuzu kucheza robo fainali kufuatia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Wauza Matairi, Misosi wanaungana na timu ya Faru Jeuri, Temeke Market, Tabata United, Makumba FC na Gomz United ambazo tayari zimefuzu kwenye hatua hiyo.

Mchezaji bora wa mchezo huo ni Idd Suleiman kutoka timu ya Misosi FC aliyejinyakulia shilingi 50,000 kutoka gazeti la michezo la Mwanaspoti. Timu ya Wauza Matairi imepata shilingi 150,000 (wamekatwa 50,000 kutokana na kuchelewa kufika uwanjani) huku Misosi FC wakiweka mfukoni shilingi 300,000 kutoka kwa Starstimes wadhamini wengine wa michuano hiyo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here